DC Kilolo awatakia mitihani mema wanafunzi wa darasa la saba,

October 7, 2020

MKUU wa wiaya ya Kilolo , Asia Abdalah ametuma salamu za kuwatakia mtihani mwema wanafunzi wa darasa la saba wanaofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wa wilaya hiyo na Tanzania kwa ujumla walioanza mitihani yao leo.

Akizungumza wakati wa kukagua zoezi la mitihani wakati alipotembelea shule za msingi Iwindi na Luganga, Asia Abdalah alisema kuwa anawatakia Kheri, Afya na Ufaulu katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi wanafunzi wote wa darasa la saba katika shule zote wilayani Kilolo na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kuwa mitihani hiyo iliyoanza leo, Wanafunzi wote wa Darasa la Saba wa Wilaya ya Kilolo wamejiandaa vyema kutokana na kazi nzuri za walimu katika wilaya hiyo na kuwataka wanafunzi kufanya mitihani hiyo kwa utulivu wa akili kuweza kufanya vyema na kuiletea sifa wilaya ya Kilolo.

“Nawatakia Mtihani mwema Wanafunzi wote wa wanaoanza Mitihani yao Leo, MUNGU wetu aliyemwaminifu awasaidie na awashindie katika mitihani yenu ,Mungu akawafanye Vichwa na Sio Mikia, Mungu awakumbushe kuandika majibu sahihi, Mungu akatoweshe magonjwa na roho za uoga wakati huu wa mitihani.” Alisema

Alisema kuwa ana amini walimu wamefanya kazi yao kwa kipindi cha miaka saba shuleni kwa wanafunzi hao na sasa ni wakati wa wanafunzi kuhakisha kwamba waliyojifunza kwenda kuyafanyia kazi katika mitihani hiyo ili waweze kufaulu vizuri na kuiletea sifa wilaya ya Kilolo na wazazi wao kwani elimu ya msingi ndio mwanzo wa maisha mazuri endapo watafanya vyema.

Alisema kuwa endapo mwanafunzi akitulia katika kufanya mitihani hiyo kuna uhakika mkubwa wa kufanya vyema na kufaulu kwani mitihani hiyo inatolewa katika masomo ambayo wamefundishwa kipindi chote wakiwa shuleni ni suala la kujiamini na utulivu wa akili na kama mmejiandaa Vizuri mtapata Matokeo Chanya.

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *