Darasa la Saba Kuanza Mitihani ya Taifa Kesho

October 6, 2020

Jumla ya watahiniwa 1,024,700  wanatarajiwa kuanza mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kuanzia kesho, Oktoba 7 hadi Oktoba 8, 2020 na watahiniwa 974,532 watafanya mitihani hiyo kwa lugha ya kuswahili huku watahiniwa  49,475 wakitarajiwa kufanya kwa lugha ya Kiingereza.

 

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde, leo, Oktoba 6, 2020 wakati akizungumza na vyombo vya habari na kuongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kusambazwa kwa karatasi za mitihani, fomu maalum za ‘OMR’ za kujibia mitihani na nyaraka zote muhimu zinazohusika katika mtihani huo nchi nzima.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *