Clouds na EATV muwe mnawapanga wasanii kabla ya kuwafanyia interview, wanawaaibisha!!!

October 5, 2020

 

Karibuni clouds wamekuwa wakiandaa show na wasanii kutoka nje ya nchi.

Kimbembe kimekuwa kikijitokeza kwenye interview na wasanii hao kwani jina la Diamond limekuwa haliepukiki.

Juzi juzi kwenye kipindi cha Friday night live EATV msanii kutoka Zimbabwe king 98 kamtaja mondi mpaka kero.

Alipoulizwa kuhusu wasanii wa Tanzania wanaosikilizwa Nigeria msanii wurld alijibu ni Diamond platnumz,v money na rayvanny.

Jana msanii rema kutoka Nigeria katua bongo. Alipoulizwa kuhusu Tanzania hakusita kumtaja Diamond platnumz.

My take;naziomba hizi media muwe mnawapanga hao wasanii. Wambieni wasanii wengine kama konde, Kiba, Nandy,n.k tofauti na hapo mtaaibika vya kutosha

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *