China yaitaka Marekani kuheshimu ushindani wa kibiashara

September 17, 2020

China imeitolea mwito Marekani kuheshimu misingi na kanuni za soko la kiuchumi pamoja na ushindani wenye usawa. Hayo yameelezwa na wizara ya mambo ya nje ya China leo wakati ilipoulizwa kuhusu kampuni ya teknolojia ya ByteDance na kusema China itahitaji kuidhinisha makubalino ya mtandao wake wa TikTok nchini Marekani. Msemaji wa wizara hiyo Wang Wenbin ndiye aliyetoa kauli hiyo katika mkutano wa kawaida na vyombo vya habari.Pendekezo lililotolewa na kampuni ya ByteDance kwa kampuni ya programu ya Marekani ya Oracle Corp la kuwa mshirika wake katika masuala ya teknolojia kwenye app ya TikTok litahitaji kuidhinishwa na maafisa wa nchi zote mbili China na Marekani, kwa mujibu wa kampuni hiyo ya ByteDance.,

China imeitolea mwito Marekani kuheshimu misingi na kanuni za soko la kiuchumi pamoja na ushindani wenye usawa. 

Hayo yameelezwa na wizara ya mambo ya nje ya China leo wakati ilipoulizwa kuhusu kampuni ya teknolojia ya ByteDance na kusema China itahitaji kuidhinisha makubalino ya mtandao wake wa TikTok nchini Marekani. 

Msemaji wa wizara hiyo Wang Wenbin ndiye aliyetoa kauli hiyo katika mkutano wa kawaida na vyombo vya habari.

Pendekezo lililotolewa na kampuni ya ByteDance kwa kampuni ya programu ya Marekani ya Oracle Corp la kuwa mshirika wake katika masuala ya teknolojia kwenye app ya TikTok litahitaji kuidhinishwa na maafisa wa nchi zote mbili China na Marekani, kwa mujibu wa kampuni hiyo ya ByteDance.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *