China yafurahishwa na uamuzi wa WTO kuhusiana na vikwazo vya Marekani, on September 16, 2020 at 5:00 pm

September 16, 2020

 China imefurahishwa na uamuzi wa Shirika la Biashara Duniani WTO kwamba vikwazo vya Marekani kwa bidhaa za China mwaka 2018 havikuendana na sheria za kimataifa za biashara. Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Wengbin amesema China inafurahishwa na uamuzi huo uliotolewa na timu ya wataalam wa WTO. Wang amesema uamuzi huo unaonyesha kwamba ni Marekani ambayo hukiuka sheria za kimataifa na kujiondoa kutoka kwenye mashirika iwapo mashirika hayo hayatofuata Marekani inavyotaka. Jopo hilo lakini limezitaka China na Marekani kuutatua mzozo wao kwa njia ya mazungumzo ya pande mbili. Vikwazo hivyo vya Marekani viliwekwa na utawala wa Trump baada ya kusema kuwa kampuni za China zinanufaika kutokana na serikali kupunguza bei ya bidhaa. Kwa kujibu, China nayo iliziwekea vikwazo vikali bidhaa za Marekani.,

 

China imefurahishwa na uamuzi wa Shirika la Biashara Duniani WTO kwamba vikwazo vya Marekani kwa bidhaa za China mwaka 2018 havikuendana na sheria za kimataifa za biashara. 

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Wengbin amesema China inafurahishwa na uamuzi huo uliotolewa na timu ya wataalam wa WTO. 

Wang amesema uamuzi huo unaonyesha kwamba ni Marekani ambayo hukiuka sheria za kimataifa na kujiondoa kutoka kwenye mashirika iwapo mashirika hayo hayatofuata Marekani inavyotaka. 

Jopo hilo lakini limezitaka China na Marekani kuutatua mzozo wao kwa njia ya mazungumzo ya pande mbili. 

Vikwazo hivyo vya Marekani viliwekwa na utawala wa Trump baada ya kusema kuwa kampuni za China zinanufaika kutokana na serikali kupunguza bei ya bidhaa. 

Kwa kujibu, China nayo iliziwekea vikwazo vikali bidhaa za Marekani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *