China na India zatupiana lawama za mashambulizi mpakani, on September 8, 2020 at 1:00 pm

September 8, 2020

India imekanusha leo shutuma za China, kwamba wanajeshi wake wamevuka mpaka unaozozaniwa na kufyatua risasi za tahadhari, ikisema badala yake kuwa wanajeshi wa China ndio waliofanya vitendo hivyo wakati wa mvutano kwenye mpaka huo. Hiyo itakuwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo minne, risasi kufyatuliwa kwenye mpaka huo ulio katika eneo la Ladakh kwenye milima mirefu ya Himalaya, na kuvunja makubaliano yaliyosainiwa baina ya China na India kupiga marufuku matumizi ya silaha za moto. Hakuna ripoti zozote juu ya vifo au majeruhi kutokana na mvutano huo. Katika taarifa yake kamandi ya magharibi ya jeshi la China imesema jeshi la India limevuka mpaka katika milima ya Shenpao, na kuongeza kuwa hatua za kutuliza hali zilichukuliwa baada ya wanajeshi hao wa India kufyatua risasi.,

India imekanusha leo shutuma za China, kwamba wanajeshi wake wamevuka mpaka unaozozaniwa na kufyatua risasi za tahadhari, ikisema badala yake kuwa wanajeshi wa China ndio waliofanya vitendo hivyo wakati wa mvutano kwenye mpaka huo. 

Hiyo itakuwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo minne, risasi kufyatuliwa kwenye mpaka huo ulio katika eneo la Ladakh kwenye milima mirefu ya Himalaya, na kuvunja makubaliano yaliyosainiwa baina ya China na India kupiga marufuku matumizi ya silaha za moto. 

Hakuna ripoti zozote juu ya vifo au majeruhi kutokana na mvutano huo. Katika taarifa yake kamandi ya magharibi ya jeshi la China imesema jeshi la India limevuka mpaka katika milima ya Shenpao, na kuongeza kuwa hatua za kutuliza hali zilichukuliwa baada ya wanajeshi hao wa India kufyatua risasi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *