China imelaani marufu ya Marekani kwa WeChat na Tik Tok, on September 19, 2020 at 1:00 pm

September 19, 2020

 China leo hii imelaani hatua ya Marekani dhidi ya programu za simu za mitandao ya kijamii za Kichina za TikTok na WeChat, ambayo inaanza kutekelezwa kesho. Kuanzia kesho raia wa Marekani hawatoweza kupakua programu hizo. Akijibu swali la mwandishi wa habari msemaji wa wizara ya biashara wa China amesema hatua hiyo inaathiri haki za kisheria za makampuni husika, kwa kuvuruga utaratibu wa kawaida wa soko. Hata hivyo amesema serikali ya China itaijibu suala hilo kwa kuchukua hatua muhimu kwa lengo la kuyalinda maslahi ya Wachina. Marufuku hiyo iliyoamriwa na Rais wa Marekani Donald Trump inatokana na kile kilichoelezwa kulinda usalama wa taifa na wasiwasi wa udukuzi wa taarifa za watu.,

 

China leo hii imelaani hatua ya Marekani dhidi ya programu za simu za mitandao ya kijamii za Kichina za TikTok na WeChat, ambayo inaanza kutekelezwa kesho. 

Kuanzia kesho raia wa Marekani hawatoweza kupakua programu hizo. Akijibu swali la mwandishi wa habari msemaji wa wizara ya biashara wa China amesema hatua hiyo inaathiri haki za kisheria za makampuni husika, kwa kuvuruga utaratibu wa kawaida wa soko. 

Hata hivyo amesema serikali ya China itaijibu suala hilo kwa kuchukua hatua muhimu kwa lengo la kuyalinda maslahi ya Wachina. 

Marufuku hiyo iliyoamriwa na Rais wa Marekani Donald Trump inatokana na kile kilichoelezwa kulinda usalama wa taifa na wasiwasi wa udukuzi wa taarifa za watu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *