Chenga ya Kisinda Yateka Mechi Chamazi…Wadai Chenga za Mauzi ziwe Zinatolewa Kadi

September 18, 2020

CHENGA aliyopiga winga wa Yanga, Tuisila Kisinda, TK Master kwenye mchezo wa wa kirafiki dhidi ya Mlandege juzi, imezua gumzo kubwa kwa mashabiki.Yanga walicheza na Mlandege juzi kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ambapo Wanajangwani hao walishinda kwa mabao 2-0.Katika mchezo huo gumzo lilitawala ilikuwa chenga aliyopiga kiungo huyo mshambuliaji wa Yanga ambapo alimfanya beki wa Mlandege kuanguka chini.Kisinda ambaye amekuwa akitajwa kuwa kati ya wachezaji mahiri zaidi kwenye timu hiyo ya Jangwani alionyesha umahiri wa kupiga chenga ambapo aliupata mpira kutoka kwa staa wa timu hiyo, Carlinhons ambapo alitisha kama anapiga shuti kali, lakini akapiga chenga ambapo beki wa Mlandege Abdallah Said alijikuta akigaragara chini.Mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Yanga juzi walikuwa wakiizungumzia chenga hiyo ambayo ilionekana kuwa bora sana pamoja na kwamba krosi yake aliyopiga haikuzaa matunda lakini mashabiki wakipagawa.Kwenye mitandao mbalimbali, chenga hiyo ilitawala jana huku baadhi ya mashabiki wa Yanga wakijisifu kutokana na kumpata mchezaji huyo aliyetokea AS Vita ya Congo.,

CHENGA aliyopiga winga wa Yanga, Tuisila Kisinda, TK Master kwenye mchezo wa wa kirafiki dhidi ya Mlandege juzi, imezua gumzo kubwa kwa mashabiki.

Yanga walicheza na Mlandege juzi kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ambapo Wanajangwani hao walishinda kwa mabao 2-0.

Katika mchezo huo gumzo lilitawala ilikuwa chenga aliyopiga kiungo huyo mshambuliaji wa Yanga ambapo alimfanya beki wa Mlandege kuanguka chini.

Kisinda ambaye amekuwa akitajwa kuwa kati ya wachezaji mahiri zaidi kwenye timu hiyo ya Jangwani alionyesha umahiri wa kupiga chenga ambapo aliupata mpira kutoka kwa staa wa timu hiyo, Carlinhons ambapo alitisha kama anapiga shuti kali, lakini akapiga chenga ambapo beki wa Mlandege Abdallah Said alijikuta akigaragara chini.

Mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Yanga juzi walikuwa wakiizungumzia chenga hiyo ambayo ilionekana kuwa bora sana pamoja na kwamba krosi yake aliyopiga haikuzaa matunda lakini mashabiki wakipagawa.Kwenye mitandao mbalimbali, chenga hiyo ilitawala jana huku baadhi ya mashabiki wa Yanga wakijisifu kutokana na kumpata mchezaji huyo aliyetokea AS Vita ya Congo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *