Chanzo cha Cardi B kudai talaka kwa mumewe Offset, on September 16, 2020 at 10:00 am

September 16, 2020

Vyanzo mbalimbali za habari za burudani zimeripoti kuhusu madai ya rapa Cardi B kwenda mahakamani na kufungua file la kudai talaka kutoka kwa mumewe ambaye ni msanii wa kundi la Migos Offset.Cardi B ameomba shauri la kudai talaka hiyo kwenye Mahakama ya Kaunti ya Fulton iliyopo Jijini Atalanta na ameeleza kuwa kwa sasa wameachana na chanzo cha kudai talaka hiyo ni kuvunjika kwa ndoa pia hakuna matarajio ya kupatanishwa.Mahakama imeamuru kuwa Offset anatakiwa kujibu shauri hilo ndani ya siku 30 na kama akishindwa kufanya hivyo basi hukumu itatoka dhidi ya rapa huyo ambaye ni mzaliwa wa Atalanta.Aidha Cardi B ametaka usawa wa kugawana mali zote ambazo wamezipata wakiwa pamoja pia anatafuta misingi ya kumkuza mtoto wao Kulture mwenye miaka miwili, na amemtaka Offset kutoa huduma zote za mtoto huyo.Cardi B na Offset wameishi pamoja miaka mitatu, walifunga ndoa ya siri Septemba 2017, na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Kulture mwenye umri wa miaka miwili.,

Vyanzo mbalimbali za habari za burudani zimeripoti kuhusu madai ya rapa Cardi B kwenda mahakamani na kufungua file la kudai talaka kutoka kwa mumewe ambaye ni msanii wa kundi la Migos Offset.

Cardi B ameomba shauri la kudai talaka hiyo kwenye Mahakama ya Kaunti ya Fulton iliyopo Jijini Atalanta na ameeleza kuwa kwa sasa wameachana na chanzo cha kudai talaka hiyo ni kuvunjika kwa ndoa pia hakuna matarajio ya kupatanishwa.

Mahakama imeamuru kuwa Offset anatakiwa kujibu shauri hilo ndani ya siku 30 na kama akishindwa kufanya hivyo basi hukumu itatoka dhidi ya rapa huyo ambaye ni mzaliwa wa Atalanta.

Aidha Cardi B ametaka usawa wa kugawana mali zote ambazo wamezipata wakiwa pamoja pia anatafuta misingi ya kumkuza mtoto wao Kulture mwenye miaka miwili, na amemtaka Offset kutoa huduma zote za mtoto huyo.

Cardi B na Offset wameishi pamoja miaka mitatu, walifunga ndoa ya siri Septemba 2017, na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Kulture mwenye umri wa miaka miwili.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *