Chanjo ya Urusi yapelekwa Venezuela kwa ajili ya majaribio,

October 4, 2020

 Makamu wa Rais wa Venezuela Delcy Rodriguez ametangaza kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona iliyotengenezwa nchini Urusi tayari imewasilishwa nchini Venezuela kwa ajili ya kufanyiwa majaribio ya awamu ya tatu.

Rodriguez ametoa taarifa kwa waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Simon Bolivar katika mji mkuu wa Caracas, ambapo chanjo hiyo ya “Sputnik V” iliyotengenezwa na Urusi ilipowasilishwa nchini Venezuela.

“Huu ni wakati wa kihistoria kwa nchi yetu, Venezuela imekuwa nchi ya kwanza Amerika kujaribu chanjo ya Urusi. Haya ni matokeo ya mawasiliano na ushirikiano mzuri kati ya Venezuela na Urusi.”, alisema Rodriguez.

Waziri wa Afya Carlos Alvarado amesema kuwa Sputnik V itajaribiwa kwa watu elfu 2 kwa siku kadhaa na kisha chanjo hiyo itazalishwa nchini Venezuela ikiwa itaonyesha mafanikio.

Ugonjwa wa Covid-19 umepelekea vifo vya watu 635 nchini Venezuela huku wengine zaidi ya elfu 76 wakiwa wamepata maambukizi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *