Chama tawala cha Japan chamchagua Suga kama Kiongozi wake mpya, on September 14, 2020 at 1:00 pm

September 14, 2020

 Chama tawala cha Japan leo Jumatatu kimemchagua katibu mkuu wa baraza la mawaziri Yoshihide Suga kama kiongozi wake mpya huku kuchaguliwa kwake kukimfanya awe na uhakika wa kuchukua nafasi ya Shinzo Abe kama waziri mkuu wa nchi hiyo.Suga alishinda kura hiyo kwa urahisi, kwa kupata kura 377 kati ya jumla ya kura 534 kutoka kwa wabunge wa chama cha Liberal Democratic na wawakilishi wa mikoa.Suga aliwashinda kwa mbali Wapinzani wake wakiwemo waziri wa zamani wa ulinzi Shigeru Ishiba na mkuu wa sera wa chama cha LDP Fumio Kishida.Kwa kuzingatia idadi kubwa ya wabunge wa LDP, Suga pia anatarajiwa kushinda kura ya bunge Jumatano na kuwa waziri mkuu, akichukua nafasi ya Abe, ambaye anajiuzulu kwa sababu za kiafya.Suga mwenye umri wa miaka 71 ambaye pia ni mshauri na msemaji wa serikali, anaonekana kuwa mtu atakaehakikisha utulivu na muendelezo wa sera za waziri mkuu anaeondoka Shinzo Abe.,

 

Chama tawala cha Japan leo Jumatatu kimemchagua katibu mkuu wa baraza la mawaziri Yoshihide Suga kama kiongozi wake mpya huku kuchaguliwa kwake kukimfanya awe na uhakika wa kuchukua nafasi ya Shinzo Abe kama waziri mkuu wa nchi hiyo.

Suga alishinda kura hiyo kwa urahisi, kwa kupata kura 377 kati ya jumla ya kura 534 kutoka kwa wabunge wa chama cha Liberal Democratic na wawakilishi wa mikoa.Suga aliwashinda kwa mbali Wapinzani wake wakiwemo waziri wa zamani wa ulinzi Shigeru Ishiba na mkuu wa sera wa chama cha LDP Fumio Kishida.

Kwa kuzingatia idadi kubwa ya wabunge wa LDP, Suga pia anatarajiwa kushinda kura ya bunge Jumatano na kuwa waziri mkuu, akichukua nafasi ya Abe, ambaye anajiuzulu kwa sababu za kiafya.

Suga mwenye umri wa miaka 71 ambaye pia ni mshauri na msemaji wa serikali, anaonekana kuwa mtu atakaehakikisha utulivu na muendelezo wa sera za waziri mkuu anaeondoka Shinzo Abe.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *