Chama Aanza Kuiota Michuano ya CAF

October 19, 2020

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama ana matumaini makubwa ya timu yao kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Novemba 20, mwaka huu ambapo michezo ya hatua ya awali itapigwa.Kwa msimu wa 2020/21, Simba ndiyo wawakilishi pekee wa michuano hiyo.

 

Akizungumzia nafasi ya Simba kwenye michuano hiyo, Chama alisema: “Nawapongeza viongozi kwa kufanya usajili bora, ukiachana na mashindano mengine tutakayoshiriki, tunafahamu tuna kibarua cha Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Zimebaki siku chache kabla ya kuanza michuano hiyo, naona kila mchezaji hapa anajitahidi kuboresha kiwango chake ili kuingia kwenye kikosi cha kwanza.

Naamini ubora wa kikosi cha msimu huu na funzo la kuaga mashindano mapema msimu uliopita ni vitu vitakavyotufanya tufanye vizuri.”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *