CHADEMA Yaahidi Kuweka Mazingira Mazuri Kwa Wafanyabiashara, on September 17, 2020 at 2:13 pm

September 17, 2020

 Na John Walter- BABATIMgombea mwenza wa Tundu Lissu kwa tiketi ya  Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu, amehaidi kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara wote.Alitoa ahadi hiyo jana Mjini Babati Mkoa wa Manyara  wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Motel Papaa.”Suala la kukadiliwa kodi kwa macho ni marufuku na maofisa wa TRA wengine hawajawahi  kumiliki hata kibanda cha nyanya,”alisema MwalimuAidha alisema mfanyabiashara hawezi kulinda biashara kwa kupigwa nyundo kichwani na maofisa wa bodi wasiokuwa waaminifu.Mwanasiasa huyo alifafanua kuwa haki za wafanyabiashara zinatakiwa kulindwa kwa kuwa wanatunza kumbukumbu za biashara zao.Alisema wengi wao wanafungua maduka yao kwa mazoea huku akiwahakikishia  kufurahia kipindi cha uongozi wa Tundu Lissu.Alitumia fursa hiyo kumuombea kura Lissu, wabunge na madiwani wa upinzani hasa wa Chadema.,


 Na John Walter- BABATI
Mgombea mwenza wa Tundu Lissu kwa tiketi ya  Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu, amehaidi kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara wote.

Alitoa ahadi hiyo jana Mjini Babati Mkoa wa Manyara  wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Motel Papaa.

“Suala la kukadiliwa kodi kwa macho ni marufuku na maofisa wa TRA wengine hawajawahi  kumiliki hata kibanda cha nyanya,”alisema Mwalimu

Aidha alisema mfanyabiashara hawezi kulinda biashara kwa kupigwa nyundo kichwani na maofisa wa bodi wasiokuwa waaminifu.

Mwanasiasa huyo alifafanua kuwa haki za wafanyabiashara zinatakiwa kulindwa kwa kuwa wanatunza kumbukumbu za biashara zao.

Alisema wengi wao wanafungua maduka yao kwa mazoea huku akiwahakikishia  kufurahia kipindi cha uongozi wa Tundu Lissu.

Alitumia fursa hiyo kumuombea kura Lissu, wabunge na madiwani wa upinzani hasa wa Chadema.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *