Chadema Iringa Yalia Na Hujuma Za Wasiojulikana, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 4, 2020

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa, William Mungai alipokuwa akizungumza na wanahabari leo (hawapo pichani)Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Iringa kimelia na hujuma zinazofanywa na wasiojulikana kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.Akizungumza na wanahabari leo Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Iringa, William Mungai amesema miongoni mwa wanazofanyiwa wagombea wao ni pamoja na kuvamiwa njiani, kupigwa na kunyang’nywa fomu wanapokuwa wakizirudisha.Mungai alipokuwa akizungumza na makamanda wa chama hicho baada ya kumaliza mkutano huo.Katika matukio hayo, Mungai amesema hivi karibuni la mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilolo akiwa anaingia amekaribia ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kurudisha fomu alivamiwa na vijana watatu ambao walimshambulia na kutaka kumnyang’anya fomu hizo.Mungai amesema hata hivyo mgombea huyo kwa kushirikiana na wanachama wa chama hicho waliokuwa eneo hilo walishirikiana na kumuokoa mgombea huyo na kuziokoa fomu hizo.Mungai alivyowasili kwenye mkutano huo.Kufuatia matukio hayo, Mungai ameliomba jeshi la polisi mkoani humo kuwasaidia kuwasaka waharifu hao ili sheria iweze kufuata mkondo wake na kufanyika uchaguzi salama na amani.,

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa, William Mungai alipokuwa akizungumza na wanahabari leo (hawapo pichani)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Iringa kimelia na hujuma zinazofanywa na wasiojulikana kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari leo Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Iringa, William Mungai amesema miongoni mwa wanazofanyiwa wagombea wao ni pamoja na kuvamiwa njiani, kupigwa na kunyang’nywa fomu wanapokuwa wakizirudisha.

Mungai alipokuwa akizungumza na makamanda wa chama hicho baada ya kumaliza mkutano huo.

Katika matukio hayo, Mungai amesema hivi karibuni la mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilolo akiwa anaingia amekaribia ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kurudisha fomu alivamiwa na vijana watatu ambao walimshambulia na kutaka kumnyang’anya fomu hizo.

Mungai amesema hata hivyo mgombea huyo kwa kushirikiana na wanachama wa chama hicho waliokuwa eneo hilo walishirikiana na kumuokoa mgombea huyo na kuziokoa fomu hizo.

Mungai alivyowasili kwenye mkutano huo.

Kufuatia matukio hayo, Mungai ameliomba jeshi la polisi mkoani humo kuwasaidia kuwasaka waharifu hao ili sheria iweze kufuata mkondo wake na kufanyika uchaguzi salama na amani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *