CEO Mpya Simba Ataja Mikakati Yake

September 10, 2020

MTENDAJI mpya wa Simba, Barbara Gonzalez, ametaja vipaumbele vyake mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuwa mtendaji wa klabu hiyo kwa kusema atahakikisha anaongeza mapato katika klabu hiyo kupitia viingilio ikiwa pamoja na kusimamia timu hiyo kufanya vyema kimataifa.Simba imemtangaza Barbara kuwa mtendaji mpya wa klabu hiyo, hivi karibuni baada ya Senzo Mazingisa kuhamia Yanga ambapo anatarajia kufanya mabadiliko kuelekea msimu mpya wa ligi kuu.Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barbara alisema kuwa moja ya mikakati yake ni kuhakikisha anaboresha uhusiano mzuri kati ya Simba na mazingira yanayoizunguka klabu hiyo.“Moja ya mikakati yangu ni kuhakikisha naboresha uhusiano mzuri wa klabu kwenye vyombo vya habari, kuitangaza klabu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya klabu kwa ujumla, mimi nitasimamia masuala yote ya klabu na mwalimu yeye atasimamia masuala ya benchi la ufundi, pia nahitaji kuhakikisha naongeza mapato ya uwanjani.“Moja ya kazi ya mwalimu Sven Vandenbroeck anayotakiwa kuifanya msimu huu ni kuhakikisha anaisimamia timu ili ichukue makombe yote ambayo tutashiriki msimu huu kuanzia ligi, Shirikisho Azam na yote tutakayocheza lakini kwa upande wa michuano ya kimataifa tumelenga kuona timu inaingia katika hatua ya makundi kisha masuala mengine yatafuata,” alisema.,

MTENDAJI mpya wa Simba, Barbara Gonzalez, ametaja vipaumbele vyake mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuwa mtendaji wa klabu hiyo kwa kusema atahakikisha anaongeza mapato katika klabu hiyo kupitia viingilio ikiwa pamoja na kusimamia timu hiyo kufanya vyema kimataifa.

Simba imemtangaza Barbara kuwa mtendaji mpya wa klabu hiyo, hivi karibuni baada ya Senzo Mazingisa kuhamia Yanga ambapo anatarajia kufanya mabadiliko kuelekea msimu mpya wa ligi kuu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barbara alisema kuwa moja ya mikakati yake ni kuhakikisha anaboresha uhusiano mzuri kati ya Simba na mazingira yanayoizunguka klabu hiyo.

“Moja ya mikakati yangu ni kuhakikisha naboresha uhusiano mzuri wa klabu kwenye vyombo vya habari, kuitangaza klabu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya klabu kwa ujumla, mimi nitasimamia masuala yote ya klabu na mwalimu yeye atasimamia masuala ya benchi la ufundi, pia nahitaji kuhakikisha naongeza mapato ya uwanjani.

“Moja ya kazi ya mwalimu Sven Vandenbroeck anayotakiwa kuifanya msimu huu ni kuhakikisha anaisimamia timu ili ichukue makombe yote ambayo tutashiriki msimu huu kuanzia ligi, Shirikisho Azam na yote tutakayocheza lakini kwa upande wa michuano ya kimataifa tumelenga kuona timu inaingia katika hatua ya makundi kisha masuala mengine yatafuata,” alisema.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *