Carlinhos Amchomoa Kiungo Yanga

September 18, 2020

UPO uwezekano mkubwa kiungo mmoja kati ya watano waliokuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha Mserbia, Zlatko Krmpotic nafasi yake kuchukuliwa na kiungo fundi raia wa Angola, Carlos Carlinhos.Hiyo ni siku chache baada ya Carlinhos kucheza kwa kiwango cha juu na kuisaidia timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Mkapa, Dar.Kiungo huyo katika mchezo huo aliingia uwanjani dakika ya 60, akatoa asisti iliyozaa bao pekee lililofungwa na Lamine Moro kwa kichwa na Yanga kushinda 1-0.Staa huyo mpya ndani ya kikosi cha Yanga, aliingia uwanjani akichukua nafasi ya kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na kufanya balaa hilo.Muangola huyo anatajwa kuingia katika kikosi cha kwanza akichukua nafasi moja kati ya viungo waliokuwepo katika kikosi cha kwanza ambao ni Haruna Niyonzima, Tuisila Kisinda, Fei Toto na Deus Kaseke anayetajwa kuwa chaguo la kwanza kutoka kikosini.Akitokea benchi, kiungo huyo alifanikiwa kupiga mashuti manne, kona tano, kati ya hizo moja ilizaa bao baada ya kuichonga kiufundi kabla ya kuingia wavuni na kuiwezesha timu yake kupata pointi tatu.Akizungumzia nafasi ya kiungo huyo, Krmpotic alisema: “Carlinhos ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa ambaye ana faida nyingi katika timu, la-kini nime-kuwa ni-kimuanzisha nje kutokana kutofanya mazoezi kwa zaidi ya mie-zi minne.“Hiyo ni baada ya ligi ya nchini kwao Angola kufutwa, hivyo ninahofia kumuharibia uwezo wake, alikuwa na program maalum kwa ajili ya kumuongezea fitinesi ambayo tayari imemalizika.“Hivyo, ninatarajia kuanza kumtumia katika kikosi cha kwanza kwenye michezo inayofuata kwani kadiri siku zinavyokwenda ndiyo anazidi kubadilika.”SIMBA WAMZUNGUMZIA CARLINHOSWakati Yanga waki-anza kutamba kutokana na kiungo huyo kuanza kuonesha cheche zake, kocha wa zamani wa Simba na mchezaji wa timu hiyo, Jamhuri Kih-welo ‘Julio’, amemzun-gumzia Carlinhos akisema kwamba ni mapema mno kuan-za kumpa ufalme.“Tatizo la Watanzania wanataka kuzungumzia adhabu ya kaburi kabla hawajakufa ama wanataka kwenda peponi huku wanaogopa kufa, Corlinhos amekuja kutoka huko alikotoka na Yanga wenyewe wanajua wametumia njia gani hadi kumpata.“Watanzania hawana utaratibu wa kusema wao wanakwenda kumfuatilia mchezaji fulani nje kwa ajili ya kumchukua, si Simba wala Yanga, hawana utaratibu huo, hivyo hakuna mtu yeyote anayemjua, wao wanakurupuka wanaletewa wachezaji au wanapewa video na wao wanasajili wachezaji. “Kinachotakiwa, ifike mahali timu ziende kuangalia wachezaji wao wenyewe ndio wawasajili.“Huwezi kumjaji Carlinhos kuwa ni mbaya ama mzuri wakati mtu mwenyewe kaja juzi na amecheza mechi chache, hatujui kiwango chake. Uwezo wa mchezaji huwezi kuufahamu akiwa amecheza mechi chache, watu wasishangilie tu na badala yake wasubiri apewe muda zaidi wa kucheza na kama ana uwezo atauonesha.“Mimi kama mwalimu mzoefu na mwenye taaluma yangu siwezi kumsifia Carlinhos kwa sababu alipiga pasi nyingi na kusababisha bao la jioni, lazima apewe muda kama wachezaji wengine ndipo aweze kusifiwa,” alisema Julio,

UPO uwezekano mkubwa kiungo mmoja kati ya watano waliokuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha Mserbia, Zlatko Krmpotic nafasi yake kuchukuliwa na kiungo fundi raia wa Angola, Carlos Carlinhos.

Hiyo ni siku chache baada ya Carlinhos kucheza kwa kiwango cha juu na kuisaidia timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kiungo huyo katika mchezo huo aliingia uwanjani dakika ya 60, akatoa asisti iliyozaa bao pekee lililofungwa na Lamine Moro kwa kichwa na Yanga kushinda 1-0.Staa huyo mpya ndani ya kikosi cha Yanga, aliingia uwanjani akichukua nafasi ya kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na kufanya balaa hilo.

Muangola huyo anatajwa kuingia katika kikosi cha kwanza akichukua nafasi moja kati ya viungo waliokuwepo katika kikosi cha kwanza ambao ni Haruna Niyonzima, Tuisila Kisinda, Fei Toto na Deus Kaseke anayetajwa kuwa chaguo la kwanza kutoka kikosini.

Akitokea benchi, kiungo huyo alifanikiwa kupiga mashuti manne, kona tano, kati ya hizo moja ilizaa bao baada ya kuichonga kiufundi kabla ya kuingia wavuni na kuiwezesha timu yake kupata pointi tatu.

Akizungumzia nafasi ya kiungo huyo, Krmpotic alisema: “Carlinhos ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa ambaye ana faida nyingi katika timu, la-kini nime-kuwa ni-kimuanzisha nje kutokana kutofanya mazoezi kwa zaidi ya mie-zi minne.

“Hiyo ni baada ya ligi ya nchini kwao Angola kufutwa, hivyo ninahofia kumuharibia uwezo wake, alikuwa na program maalum kwa ajili ya kumuongezea fitinesi ambayo tayari imemalizika.

“Hivyo, ninatarajia kuanza kumtumia katika kikosi cha kwanza kwenye michezo inayofuata kwani kadiri siku zinavyokwenda ndiyo anazidi kubadilika.”

SIMBA WAMZUNGUMZIA CARLINHOS

Wakati Yanga waki-anza kutamba kutokana na kiungo huyo kuanza kuonesha cheche zake, kocha wa zamani wa Simba na mchezaji wa timu hiyo, Jamhuri Kih-welo ‘Julio’, amemzun-gumzia Carlinhos akisema kwamba ni mapema mno kuan-za kumpa ufalme.

“Tatizo la Watanzania wanataka kuzungumzia adhabu ya kaburi kabla hawajakufa ama wanataka kwenda peponi huku wanaogopa kufa, Corlinhos amekuja kutoka huko alikotoka na Yanga wenyewe wanajua wametumia njia gani hadi kumpata.

“Watanzania hawana utaratibu wa kusema wao wanakwenda kumfuatilia mchezaji fulani nje kwa ajili ya kumchukua, si Simba wala Yanga, hawana utaratibu huo, hivyo hakuna mtu yeyote anayemjua, wao wanakurupuka wanaletewa wachezaji au wanapewa video na wao wanasajili wachezaji. “Kinachotakiwa, ifike mahali timu ziende kuangalia wachezaji wao wenyewe ndio wawasajili.

“Huwezi kumjaji Carlinhos kuwa ni mbaya ama mzuri wakati mtu mwenyewe kaja juzi na amecheza mechi chache, hatujui kiwango chake. Uwezo wa mchezaji huwezi kuufahamu akiwa amecheza mechi chache, watu wasishangilie tu na badala yake wasubiri apewe muda zaidi wa kucheza na kama ana uwezo atauonesha.

“Mimi kama mwalimu mzoefu na mwenye taaluma yangu siwezi kumsifia Carlinhos kwa sababu alipiga pasi nyingi na kusababisha bao la jioni, lazima apewe muda kama wachezaji wengine ndipo aweze kusifiwa,” alisema Julio

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *