Carlinhos Akiona Yanga SC, Akimbizwa Saa Zima, noreply@blogger.com (Udaku Special)

August 28, 2020

STAA mpya wa Yanga, Muangola, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo ‘Carlinhos’, jana Alhamisi alionja joto ya jiwe baada ya kukimbizwa kwa takribani saa nzima katika mazoezi ya kikosi hicho.Muangola huyo alikutana na hali hiyo ikiwa ni siku ya pili tu baada ya kuanza mazoezi ya kikosi hicho baada ya kujiunga na Yanga akitokea Interclub ya kwao kwa mkataba wa miaka miwili.Carlinhos na mastaa wengine jana waliendelea na mazoezi yao kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar ikiwa ni kujiandaa na mechi ya kilele cha Wiki ya Mwananchi ambacho kitafanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa MkapaMuangola huyo alifanyishwa mazoezi hayo ya kukimbia kwa kuzunguka uwanja mzima kwa lengo la kumuweka fi ti huku akisimamiwa na kocha mpya msaidizi Juma Mwambusi na kocha wa viungo Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini.Katika kundi la mastaa ambao walikuwa sambamba na Carlinhos katika zoezi hilo la kukimbia ni pamoja na Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko, Waziri Junior, Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yassin Mustapha na Deus Kaseke.Wakati wachezaji hao wakiwa wanafanya zoezi hilo wachezaji wengine walikuwa wakiendelea na program nyingine zikiwemo za kuchezea mpira ndani ya uwanja.,

STAA mpya wa Yanga, Muangola, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo ‘Carlinhos’, jana Alhamisi alionja joto ya jiwe baada ya kukimbizwa kwa takribani saa nzima katika mazoezi ya kikosi hicho.

Muangola huyo alikutana na hali hiyo ikiwa ni siku ya pili tu baada ya kuanza mazoezi ya kikosi hicho baada ya kujiunga na Yanga akitokea Interclub ya kwao kwa mkataba wa miaka miwili.

Carlinhos na mastaa wengine jana waliendelea na mazoezi yao kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar ikiwa ni kujiandaa na mechi ya kilele cha Wiki ya Mwananchi ambacho kitafanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Mkapa

Muangola huyo alifanyishwa mazoezi hayo ya kukimbia kwa kuzunguka uwanja mzima kwa lengo la kumuweka fi ti huku akisimamiwa na kocha mpya msaidizi Juma Mwambusi na kocha wa viungo Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini.

Katika kundi la mastaa ambao walikuwa sambamba na Carlinhos katika zoezi hilo la kukimbia ni pamoja na Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko, Waziri Junior, Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yassin Mustapha na Deus Kaseke.

Wakati wachezaji hao wakiwa wanafanya zoezi hilo wachezaji wengine walikuwa wakiendelea na program nyingine zikiwemo za kuchezea mpira ndani ya uwanja.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *