Bwana Rusesabagina ni miongoni mwa majina yaliyopo kwenye waranti ya kimataifa

September 6, 2020

Dakika 3 zilizopita

Rais Paul Kagame

Kwa mara ya kwanza Rais wa Rwanda Paul Kagame amezungumzia kwa mara ya kwanza madai ya kutekwa kwa mkosoaji wa bwana Kagame Paul Rusesabagina

Akizungumza kuhusu madai ya kutekwa jinsi Paul Rusesabagina alijikuta Rwanda, Rais Paul Kagame amesema ilikuwa ”zaidi kuhusu yeye binafsi kuliko mtu mwingine yeyote”.

Katika matangazo ya moja kwa moja kwa televisheni ya taifa Jumapili jioni, Bwana Kagame amesema kwamba hajali kuhusu hadithi ya Bwana Rusesabagina kwamba yeye ni shujaa wa mauaji ya kimbari na kwamba ”hilo si jambo ambalo litakalomkabili mahakamani”.

Bwana Kagame amesema kuwa Paul Rusesabagina alikuwa kiongozi wa makundi ya watu wenye silaha, FNL miongoni mwao, na ambapo hivi karibuni lilianzisha mshambulizi dhidi ya Rwanda na ”kuua watu Kusini Magharibi”.

” Rusesabagina ametoa maelezo kabla hajafika hapa, mwenyewe akisifia jambo hilo.” Rais Kagame alisema.

Paul Rusesabagina, ni kiongozi wa muungano wa kisasa MRCD-Ubumwe ambacho Rwanda inauhusisha na mashambulio ya ugaidi yaliyowaua Wanyarwanda katika kituo cha polisi cha mjini Kigali.

Hajazungumza chochote kuhusu madai dhidi yake.

Rwanda inasema Paul Rusesabagina alikamatwa kufuatia "ushirikiano wa kimataifa "

Familia ya Bwana Rusesabagina na chama wamesema kuwa alitekwa nyara mwishoni mwa juma lililopita alipokuwa katika safari binafsi kuelekea Dubai, na kufikishwa mjini Kigali nchini Rwanda.

Akizungumza na BBC mtoto wa kike wa Bwana Rusesabagina -Anaïse Kanimba alisema :”alitekwa nyara alipokuwa safarini Dubai “, katika Muungano wa nchi za kiarabu (UAE).”

“Alifika Jumanne, ndio mara ya mwisho tulipozungumza nae akituambia kuwa amefika salama, hatukumsikia tena hadi tulipoona kuwa amekamatwa na utawala wa Rwanda.

“Hatujui alifikaje huko na kilichotokea, ndio maana tunafikiria kuwa alitekwa kwasababu asingeenda Rwanda kwa hiari yake.”

Anaishi uhamishoni Marekani na ni raia wa ubelgiji , aliongeza.

Source link

,Dakika 3 zilizopita Chanzo cha picha, RTV/LIVE EVENT Kwa mara ya kwanza Rais wa Rwanda Paul Kagame amezungumzia kwa mara…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *