Bushangama aliokoa maisha ya watoto walioungua moto akiamini mwanae yu hai

September 16, 2020

Dakika 2 zilizopita

Najibu saidi Bushangama, ambaye aliokoa watoto wa wenzie watano bila kufahamu kwamba mtoto wake alikua miongoni mwa walioteketea

Ilikuwa siku yenye taharuki kubwa kwa bwana Najibu saidi Bushangama, ambaye aliokoa watoto wa wenzie watano bila kufahamu kwamba mtoto wake alikua miongoni mwa walioteketea

Kijana wake Alfa Alauni ni miongoni mwa Wanafunzi 10 waliofariki dunia pale moto ulipoteketeza bweni la shule yao ya Byamungu English Medium iliyoko wilayani Kyerwa, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania

Najibu Said Bushangama anakaa umbali wa mita mia mbili kutoka shuleni ambapo tukio la ajali ya moto lilitokea.

Ilikuwa hali ya taharuki kubwa kwa bwana Bushangama kutokana na tukio hilo lililotokea wilayani Kyerwa..

”Nilikuwa nyumbani , kuna kaka yangu alikuwa karibu na shule akaniita saa sita usiku akaniambia shule imeungua nikaamka nikaambiwa nichukue gari kwa ajili ya kuchua majeruhi kuwapeleka hospitali”. bwana Bushangama aliiambia BBC.

Bwana Bushangama anasema alipofika katika eneo la tukio alikuta paa la jengo limekwisha poromoka.

Bila kuwa na uhakika alipo mwanae ambaye alikuwa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo ,aliwabeba majeruhi, watoto watano ili kuwakimbiza hospitali ya Nyakahanga.

Anasema alifanya mawasiliano na wazazi wa watoto hao kuwataka wafie

”Baada ya kutoka hospitali na kurudi katika eneo la shule ndipo nilipogundua kuwa mtoto wangu aliungua na moto.” Alisema Bwana Bushangama.

Baba yake Alfa alidokezwa kuwa Alfa alikuwa ametoka na kukimbia, jibu lililokuwa limempa matumaini kuwa mtoto wake ni mzima wa afya.

Kilichokuwa kikisubiriwa ni matokeo ya vipimo vya vinasaba kuweza kubaini watoto wao vilivyochukuliwa siku ya Jumatatu.

”Waliniuliza hospitali Alfa unaye kati ya majeruhi uliowaleta?, nikajibu sinaye, hapo nikahisi kuwa mtoto wangu atakuwa ameungua.”

Mara ya mwisho alimuona mtoto wake wakati alipokuwa akijiandaa kusafiri kwenda kumuona mkewe

Hivyo alimtembelea Alfa na kumpa simu ili azungumze na mama yake anasema ilikuwa kamam alikuwa anamuaga kwa mara ya mwisho.

Hivi sasa anachosubiri ni matokeo ya vipimo vya vinasaba vilivyochukuliwa ili kuweza kubaini miili ya watoto wao vilivyochukuliwa siku ya Jumatatu.

Source link

,Dakika 2 zilizopita Chanzo cha picha, Najibu Saidi Bushangama Ilikuwa siku yenye taharuki kubwa kwa bwana Najibu saidi Bushangama, ambaye…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *