Burundi na Tanzania kuimarisha uhusiano

September 19, 2020

Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye leo 19 Septemba amefanya zaira yake rasmi nchini na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, Hafla ya ukaribisho imefanyika katika uwanja wa  Lake Tanganyika mkoani Kigoma, ambapo Marais wote hao wawili wamehutubia wananchi na kuelezea nia ya kushirikiana kibiashara kwa mataifa yote mawili.”Biashara kati ya nchi hizi mbili zimeanza kuongezeka, mwaka 2016 biashara kati ya nchi hizi mbili ilikuwa bilion 115.15 kwa sasa hivi imeongezeka na kufikia bilioni 201, lakini pia kituo chetu cha uwekezaji kimesajili miradi 16 kutoka Burundi ambayo inathamani ya SPLA za Marekani Milioni 29.42 naimetoa ajira zaidi ya watu 544, lakini pia tunataarifa kuwa zaidi ya makampuni 10 kutoka Tanzania nayo yamewekeza Burundi”, amesema Dkt Magufuli.Katika ushirikiano huo wa kibiashara kati ya nchi za Burundi na Tanzania, Mkoa wa Kigoma unatarajiwa kuwa eneo la mkakati na kitovu cha biashara kati ya nchi zote mbili, huku miundombinu ya reli, usafiri wa majini na anga ukitazamiwa kuimarishwa ili kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa pande zote mbili.”Burundi tuko tayari kufanya kazi na tunaona tutapata ‘benefit’ kubwa kwa ile bandari, mmeamua kujenga reli ya kisasa ili mtusaidie na Kigoma nasikia kwamba mko mnafanya chochote ili tuweze kupata msaada wa kuendesha biashara Burundi tunawashukuru sana , nataka tena niwaambie kwamba Burundi sasa hivi hali ya usalama ni shwari sio kama zamani” Evariste Ndayishimiye, Rais wa Burundi,

Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye leo 19 Septemba amefanya zaira yake rasmi nchini na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, 

Hafla ya ukaribisho imefanyika katika uwanja wa  Lake Tanganyika mkoani Kigoma, ambapo Marais wote hao wawili wamehutubia wananchi na kuelezea nia ya kushirikiana kibiashara kwa mataifa yote mawili.

“Biashara kati ya nchi hizi mbili zimeanza kuongezeka, mwaka 2016 biashara kati ya nchi hizi mbili ilikuwa bilion 115.15 kwa sasa hivi imeongezeka na kufikia bilioni 201, lakini pia kituo chetu cha uwekezaji kimesajili miradi 16 kutoka Burundi ambayo inathamani ya SPLA za Marekani Milioni 29.42 naimetoa ajira zaidi ya watu 544, lakini pia tunataarifa kuwa zaidi ya makampuni 10 kutoka Tanzania nayo yamewekeza Burundi”, amesema Dkt Magufuli.

Katika ushirikiano huo wa kibiashara kati ya nchi za Burundi na Tanzania, Mkoa wa Kigoma unatarajiwa kuwa eneo la mkakati na kitovu cha biashara kati ya nchi zote mbili, huku miundombinu ya reli, usafiri wa majini na anga ukitazamiwa kuimarishwa ili kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa pande zote mbili.

”Burundi tuko tayari kufanya kazi na tunaona tutapata ‘benefit’ kubwa kwa ile bandari, mmeamua kujenga reli ya kisasa ili mtusaidie na Kigoma nasikia kwamba mko mnafanya chochote ili tuweze kupata msaada wa kuendesha biashara Burundi tunawashukuru sana , nataka tena niwaambie kwamba Burundi sasa hivi hali ya usalama ni shwari sio kama zamani” Evariste Ndayishimiye, Rais wa Burundi

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *