Bunge la Uturuki lalaani hatua ya Armenia,

October 12, 2020

Kiongozi wa Bunge la Uturuki Mustafa Şentop, ameripoti kuwa Armenia sasa ni shida ya ulimwengu.

Mustafa Şentop, kwenye akaunti yake ya Twitter, amesema kuwa licha ya uamuzi wa kusitisha mapigano uliochukuliwa huko Moscow, mji mkuu wa Urusi, Armenia inaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Azerbaijan ikilenga raia.

Şentop amesisitiza kuwa mashambulizi haya ni uhalifu wa kivita kwa sababu yanawalenga raia moja kwa moja na kwamba Armenia inapaswa kuhukumiwa.

“Armenia sasa ni shida ya ulimwengu.”, alisema.

Armenia na Azerbaijan ziliamua kusitisha mapigano  Nagorno-Karabakh, kuanzia saa 12:00 saa za kawaida mnamo Oktoba 10, wakati wa mkutano uliyofanyika Moscow, mji mkuu wa Urusi.

Kabla hata ya masaa 24 kupita baada ya uamuzi huo kutolewa, Armenia ilifanya shambulizi la makombora katika mji wa Ganja na kupelekea vifo vya watu 9 na wengine 34 kujeruhiwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *