Breaking: Watano Wafariki Ajali ya Daladala na Lori Dar

October 5, 2020

WATU watano wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyohusisha daladala na lori la mchanga katika eneo la Chang’ombe jijini Dar es Salaam iliyotokea alfajiri ya leo Jumatatu, Oktoba 5, 2020.

 

 

Kamanda wa Polisi Temeke jijini Dar es Salaam, Amon Kakwale,  na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi  kuhusu chanzo cha ajali hiyo.

Daladala hiyo hufanya safari zake  maeneo ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Updates

DAR ES SALAAM 05.10.2020

Mpaka sasa Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea majeruhi watano kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke waliopata ajali leo asubuhi  05.10.2020 eneo la Chang’ombe-Temeke.

1. William Paul Akida (Me-42)

2. Jina halijafahamika (Me-32)

3. Jina halijafahamika (Me-20)

4. Alicia Teophil (Ke-25)

5. Valentino Lucas (Ke-29)

Wanaendelea na matibabu. Haya yamethibithishwa na Aminiel Aligaesha

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano

Hospitali ya Taifa Muhimbili.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *