Breaking News: Zitto Kabwe Apata Ajali Kigoma

October 6, 2020

KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amepata ajali ya gari katika Kijiji cha Kalia, mkoani Kigoma,  akiwa njiani kuelekea kwenye mikutano ya kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini mchana wa leo, Oktoba 6, 2020.

 

Taarifa hizo zimethibitishwa kupitia akaunti ya Twitter ya ACT Wazalendo na kuongeza kwamba Zitto alikuwa na watu wengine wanne kwenye gari lililopata ajali, na kwamba kiongozi huyo amepelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi  na matibabu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *