Boti lililowabeba watafuta hifadhi wa Uturuki lawasili nchini Ugiriki, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 30, 2020 at 3:00 pm

August 30, 2020

Maboti mawili ya kuvulia samaki yaliowabeba watu wanaotafuta hifadhi 26 kutoka Uturuki yamewasili katika kisiwa cha Ugiriki cha Chios, walinzi wa Pwani ya Ugiriki wamesema hii leo. Kundi hilo lililowajumuisha watoto, liliokolewa na walinzi hao lilipokaribia ufuo huo hapo jana.Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Politischios nchini humo, raia hao wa Uturuki walikuwa wanatafuta hifadhi ya kisiasa nchini Ugiriki wakidai kuteswa na serikali ya rais Recep Tayyip Erdogan. Abiria wawili walitoboa mashimo katika boti lilipokuwa likikaribia kisiwa hicho kuchochea juhudi za uokoaji.Wawili hao walikamatwa baadaye. Kundi la watu hao lilipimwa virusi vya corona na kuhamishiwa katika kituo cha karantini cha Lefkonia. Visa wa raia wa Uturuki wengi wao wakiwa watumishi wa umma na maafisa wa kijeshi wanaofika katika visiwa vya Ugiriki na kuingia nchini humo kupitia mpaka katika mto Evros vimeripotiwa tangu mwaka 2016 baada ya kushindwa kwa jaribio la kuipindua serikali ya rais Erdogan.,

Maboti mawili ya kuvulia samaki yaliowabeba watu wanaotafuta hifadhi 26 kutoka Uturuki yamewasili katika kisiwa cha Ugiriki cha Chios, walinzi wa Pwani ya Ugiriki wamesema hii leo. Kundi hilo lililowajumuisha watoto, liliokolewa na walinzi hao lilipokaribia ufuo huo hapo jana.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Politischios nchini humo, raia hao wa Uturuki walikuwa wanatafuta hifadhi ya kisiasa nchini Ugiriki wakidai kuteswa na serikali ya rais Recep Tayyip Erdogan. Abiria wawili walitoboa mashimo katika boti lilipokuwa likikaribia kisiwa hicho kuchochea juhudi za uokoaji.

Wawili hao walikamatwa baadaye. Kundi la watu hao lilipimwa virusi vya corona na kuhamishiwa katika kituo cha karantini cha Lefkonia. Visa wa raia wa Uturuki wengi wao wakiwa watumishi wa umma na maafisa wa kijeshi wanaofika katika visiwa vya Ugiriki na kuingia nchini humo kupitia mpaka katika mto Evros vimeripotiwa tangu mwaka 2016 baada ya kushindwa kwa jaribio la kuipindua serikali ya rais Erdogan.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *