Bosi Simba Ampa Morrison Ndinga,, Atuma Ujumbe Insta

September 15, 2020

BERNARD MORRISON kiungo mshambuliaji wa Simba ameonyesha furaha yake na kumshukuru  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji,’Mo’,  kwa kuonyesha picha ya gari ambayo inatajwa kuwa amepewa zawadi na bosi huyo wa Simba.Morrison alijiunga na Simba akitokea Yanga ambapo dili lake la usajili lilileta utata kwa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa na mabosi wake wa zamani Yanga ambao walieleza kuwa nyota huyo ana mkataba wa miaka miwili huku yeye akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita.Sakata hilo ambalo lilivuta hisia za mashabiki na wadau wa mpira lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10-12 makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na mwisho wa siku Morrison alitangazwa kuwa mshindi kutokana na makosa yaliyogundulika kwenye mkataba wake ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa tarehe ndani ya mkataba wake.Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Morrison ameonyesha picha mpya ya gari na kuandika maneno ya shukrani kwa bosi wa Simba ‘Mo’ huku akiweka ujumbe wa utani kama kijembe kwa wale ambao wanaeleza kuwa hajali wachezaji.“Asante sana Mo, ni mfano wa kiongozi mkubwa, asante Simba ni hatua nyingine, endeleeni kusema kwamba hajali wachezaji wake.”,

BERNARD MORRISON kiungo mshambuliaji wa Simba ameonyesha furaha yake na kumshukuru  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji,’Mo’,  kwa kuonyesha picha ya gari ambayo inatajwa kuwa amepewa zawadi na bosi huyo wa Simba.

Morrison alijiunga na Simba akitokea Yanga ambapo dili lake la usajili lilileta utata kwa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa na mabosi wake wa zamani Yanga ambao walieleza kuwa nyota huyo ana mkataba wa miaka miwili huku yeye akieleza kuwa ana mkataba wa miezi sita.

Sakata hilo ambalo lilivuta hisia za mashabiki na wadau wa mpira lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10-12 makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na mwisho wa siku Morrison alitangazwa kuwa mshindi kutokana na makosa yaliyogundulika kwenye mkataba wake ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa tarehe ndani ya mkataba wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Morrison ameonyesha picha mpya ya gari na kuandika maneno ya shukrani kwa bosi wa Simba ‘Mo’ huku akiweka ujumbe wa utani kama kijembe kwa wale ambao wanaeleza kuwa hajali wachezaji.

“Asante sana Mo, ni mfano wa kiongozi mkubwa, asante Simba ni hatua nyingine, endeleeni kusema kwamba hajali wachezaji wake.”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *