Boris Johnson asema Uingereza ijiandae kutoelewana na Umoja wa Ulaya katika makubaliano ya biashara

October 17, 2020

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema leo nchi hiyo lazima ijiandae kwa kutopatikana maelewano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya labda kuwepo na mabadiliko ya kimsimamo upande wa umoja huo. 

Johnson anasema Umoja wa Ulaya unakataa kuipatia nchi yake makubaliano ya kibiashara kama yale ya Canada, makubaliano ambayo Uingereza ndiyo inayoyatafuta. “Na kwa matumaini makubwa tutajiandaa kukumbatia mbadala. Tuwe tayari kwa Januari mosi yenye mpango ulio sawa na wa Australia ambao umetokana na msingi wa biashara huria duniani. 

Tutafanikiwa pakubwa kama nchi yenye kujitegemea na inayofanya biashara huru ambapo tunadhibiti mipaka yetu, uvuvi wetu na kujiwekea sheria zetu wenyewe.”Johnson alikuwa anawajibu viongozi wa Umoja wa Ulaya ambao katika mkutano wa kilele mjini Brussels walisema UIngereza inahitajika kubadili msimamo wake ili kuwe na uwezekano wa kupatikana maelewano. 

Uingereza ilikuwa imetishia kujiondoa kutoka kwenye mazungumzo hayo iwapo makubaliano ya kibiashara hayatopatikana katika mkutano huo unaoisha leo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *