“Bodyguard Siku Hizi ni Wengi Kuliko Wasanii“ – Christian Bella

October 2, 2020

 Msanii Christian Bella amewachana wasanii wanaotembea na ulinzi ‘bodyguards’ kwa sababu anaona wamekuwa wengi kuhusu kuliko wasanii wenyewe pale wanapokutana kwenye sehemu za show au kwenye shughuli zingine za kisanii.

Akizungumzia hilo kwenye show ya eNewz ya East Africa TV, Christian Bella amesema mtu hawezi kuwa na Bodyguard watano au sita wakati  nyumbani kwake anapoishi anadaiwa kodi, kitendo hicho ni kukosa fikra katika tasnia ya sanaa ya muziki.

“Mimi nimewahi kwenda kwenye show nikashangaa ‘backstage’ kila msanii ana ‘bodyguards’ na wengine wakakomoa wakaja na walinzi sita, cha kushangaza walinzi walikuwa wengi kuliko wasanii mpaka nikauliza hawa ndiyo wasanii au basi nilijikuta nacheka sana” amesema Christian Bella

“Huwezi kuwa na walinzi wengi huku unadaiwa kodi ingawa siwezi kukasirika nikimuona mtu ana bodyguard wengi ila sio kujibrand ukiwa na walinzi wengi, lifestyle na pesa ndiyo humbeba mtu sio bodyguard kwa mtazamo wangu” ameongeza

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *