Bodi ya usajili ya Wahandisi yatakiwa kuwachukulia hatua wahandisi wanaokiuka miiko, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on September 3, 2020 at 3:00 pm

September 3, 2020

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.Serikali imeitaka bodi ya usajili wa Wahandisi nchini ERB kuwachukulia hatua Wahandisi wanaokwenda kinyume na taaluma zao na kufuata matakwa yao binafsi katika kutekeleza majukumu yao.Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi wakati wakifungua mkutano wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao.Amesema Uhandisi ni Taaluma muhimu na wanataaluma wanatakiwa kuiheshimu na bodi ya usajili ihakikishe inawachukulia hatua kali za kisheria wanaokiuka miiko yao kwa sababu wameapa kufuata masharti ya taaluma.” Bodi isisite kuwachukulia hatua kali wale wanaoenda kinyume kweli ninyi ni walezi lakini hakikisheni wahandisi wanafuata masharti na wanaokiuka mnawachukulia hatua kali” amesema balozi Kijazi.Amewataka wataalamu hao kutumia taaluma yao kikamilifu na kuanzisha mifumo ya ndani ili kama nchi tusitegemee mifumo ya nje ya nchi na tutumie mifumo yetu wenyewe.Amesema Serikali ya awamu ya tano inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ili kufikia nchi ya viwanda mfano mradi wa mwalimu Nyerere wa kuzalisha umeme ambao utazalisha umeme mwingi utakao wezesha katika kuendesha viwanda.” Ninyi kama wahandisi mtumie fulsa hii ya mapinduzi ya viwanda kwa sababu taaluma hiyo itahitajika Sana hasa katika ujenzi na uendeshaji wa Viwanda hivyo na tutakuwa na umeme wa kutosha kuendesha viwanda hivyo” amesema.Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya usajili wa Wahandisi nchini (ERB) Prof. Ninatubu Lema, amesema mkutano huo ni wa siku mbili kwa wahandisi kujadili changamoto zinazowapata katika utekelezaji wa majukumu yao.Amesema katika mkutano huo wahandisi takribani 452 wataapa kiapo kwa ajili ya kuheshimu taaluma hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao katika taaluma hiyo.Amebainisha kuwa mpaka Sasa bodi hiyo imesajili wahandisi elfu ishirini na tisa(29) na malengo yao kusajili wahandisi elfu themanini (80) ifikapo 2025.,

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Serikali imeitaka bodi ya usajili wa Wahandisi nchini ERB kuwachukulia hatua Wahandisi wanaokwenda kinyume na taaluma zao na kufuata matakwa yao binafsi katika kutekeleza majukumu yao.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi wakati wakifungua mkutano wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano ulioenda sambamba na kiapo kwa wahandisi wapya katika kutumikia taaluma zao.

Amesema Uhandisi ni Taaluma muhimu na wanataaluma wanatakiwa kuiheshimu na bodi ya usajili ihakikishe inawachukulia hatua kali za kisheria wanaokiuka miiko yao kwa sababu wameapa kufuata masharti ya taaluma.

” Bodi isisite kuwachukulia hatua kali wale wanaoenda kinyume kweli ninyi ni walezi lakini hakikisheni wahandisi wanafuata masharti na wanaokiuka mnawachukulia hatua kali” amesema balozi Kijazi.

Amewataka wataalamu hao kutumia taaluma yao kikamilifu na kuanzisha mifumo ya ndani ili kama nchi tusitegemee mifumo ya nje ya nchi na tutumie mifumo yetu wenyewe.

Amesema Serikali ya awamu ya tano inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ili kufikia nchi ya viwanda mfano mradi wa mwalimu Nyerere wa kuzalisha umeme ambao utazalisha umeme mwingi utakao wezesha katika kuendesha viwanda.

” Ninyi kama wahandisi mtumie fulsa hii ya mapinduzi ya viwanda kwa sababu taaluma hiyo itahitajika Sana hasa katika ujenzi na uendeshaji wa Viwanda hivyo na tutakuwa na umeme wa kutosha kuendesha viwanda hivyo” amesema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya usajili wa Wahandisi nchini (ERB) Prof. Ninatubu Lema, amesema mkutano huo ni wa siku mbili kwa wahandisi kujadili changamoto zinazowapata katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema katika mkutano huo wahandisi takribani 452 wataapa kiapo kwa ajili ya kuheshimu taaluma hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao katika taaluma hiyo.

Amebainisha kuwa mpaka Sasa bodi hiyo imesajili wahandisi elfu ishirini na tisa(29) na malengo yao kusajili wahandisi elfu themanini (80) ifikapo 2025.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *