Berlin yajiandaa kwa maandamano makubwa ya kupinga corona, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 29, 2020 at 1:00 pm

August 29, 2020

Maelfu ya watu wenye kutia shaka kuhusu janga la virusi vya corona nchini Ujerumani wameanza kukusanyika mjini Berlin katika maandamano makubwa ya kupinga vizuizi vilivyowekwa na serikali. Maandamano hayo yameruhusiwa kufanyika baada ya mapambano makali mahakamani. Polisi imesema itaweka ulinzi na kufuatilia kanuni ya uvaaji barakoa na watu kutosogeleana. Mkuu wa polisi Berlin, Barbara Slowik ameonya kuwa kama waandamanaji hawatazingatia kanuni za usalama kuepusha maambukizi ya virusi vya corona, polisi watayavunja maandamano hayo haraka sana. Maafisa wa mji wa Berlin awali waliamua kutoyaruhusu maandamano hayo ya leo, wakihofia kuwa idadi inayokadiriwa ya waandamanaji 22,000 hawatazingatia masharti ya kukaa umbali wa mita moja na nusu au kuvaa barakoa. Lakini katika mkesha wa maandamano hayo, mahakama ya Berlin iliwaunga mkono waandamanaji, ikisema hakuna dalili kuwa waandalizi watapuuza makusudi kanuni hizo na kuhatarisha afya ya umma.,

Maelfu ya watu wenye kutia shaka kuhusu janga la virusi vya corona nchini Ujerumani wameanza kukusanyika mjini Berlin katika maandamano makubwa ya kupinga vizuizi vilivyowekwa na serikali. 

Maandamano hayo yameruhusiwa kufanyika baada ya mapambano makali mahakamani. Polisi imesema itaweka ulinzi na kufuatilia kanuni ya uvaaji barakoa na watu kutosogeleana. 

Mkuu wa polisi Berlin, Barbara Slowik ameonya kuwa kama waandamanaji hawatazingatia kanuni za usalama kuepusha maambukizi ya virusi vya corona, polisi watayavunja maandamano hayo haraka sana. 

Maafisa wa mji wa Berlin awali waliamua kutoyaruhusu maandamano hayo ya leo, wakihofia kuwa idadi inayokadiriwa ya waandamanaji 22,000 hawatazingatia masharti ya kukaa umbali wa mita moja na nusu au kuvaa barakoa. 

Lakini katika mkesha wa maandamano hayo, mahakama ya Berlin iliwaunga mkono waandamanaji, ikisema hakuna dalili kuwa waandalizi watapuuza makusudi kanuni hizo na kuhatarisha afya ya umma.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *