Belarus yatangaza kulipiza kisasi kwa kuiwekea vikwazo Umoja wa Ulaya,

October 2, 2020

 

Belarus leo imesema kuwa inauwekea Umoja wa Ulaya vikwazo kama jawabu la umoja huo kuwawekea vikwazo maafisa wake kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata uliompa tena ushindi rais Alexander Lukashenko. 

Mapema Ijumaa, viongozi wa Umoja wa Ulaya waliidhinisha vikwazo vya usafiri na kushikiliwa kwa mali za maafisa 40 wa serikali ya Belarus ambao wanasema walihusika katika wizi wa kura kwenye uchaguzi huo wa Agosti 9 na pia katika kuwashambulia waandamanaji waliokuwa wanapinga uchaguzi huo. 

Angela Merkel ni Kansela wa Ujerumani, na kiongozi wa baraza la Ulaya kwa wakati huu.”Tunaweza kusema leo kwamba vikwazo dhidi ya wahusika Belarus vitakuwa na tija, hii inamaanisha kwamba Umoja wa Ulaya unawachukulia hatua wale wanaopinga demokrasia na nafikiri hii ni ishara muhimu sana.

“Uingereza na Canada tayari zimeshawawekea vikwazo maafisa wa Belarus ila Umoja wa Ulaya haujamuwekea vikwazo Rais Alexander Lukashenko mwenyewe.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *