Belarus imeinya EU kwa kumwalika mpinzani wa Lukashenko, on September 19, 2020 at 6:00 pm

September 19, 2020

 Wizara ya mambo ya Nje ya Belarus imesema inautazama uwezekano wa ushiriki wa mwanasiasa wa upinzani, Sviatlana Tsikhanouskaya katika mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Umoja wa Ulaya, kama uingiliwaji wa masuala ya ndani ya taifa hilo. Tsikhanouskaya amekuwa mpinzani mkubwa wa Alexander Lukashenko ambae ameiongoza Belarus kwa miaka 26 sasa. Wizara ya mambo ya nje imesema imetoa taarifa kwa ulaya kuhusiana na mtazamo wake huo. Shirika la habari la Urusi liliripoti kwamba Tsikhanouskaya anatarajiwa kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya ambao unatarajiwa kufanyika juma lijalo.,

 

Wizara ya mambo ya Nje ya Belarus imesema inautazama uwezekano wa ushiriki wa mwanasiasa wa upinzani, Sviatlana Tsikhanouskaya katika mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Umoja wa Ulaya, kama uingiliwaji wa masuala ya ndani ya taifa hilo. 

Tsikhanouskaya amekuwa mpinzani mkubwa wa Alexander Lukashenko ambae ameiongoza Belarus kwa miaka 26 sasa. Wizara ya mambo ya nje imesema imetoa taarifa kwa ulaya kuhusiana na mtazamo wake huo. 

Shirika la habari la Urusi liliripoti kwamba Tsikhanouskaya anatarajiwa kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya ambao unatarajiwa kufanyika juma lijalo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *