Bayern wawazidi kete Dortmund Super Cup

October 1, 2020

Haya ni licha ya hofu kuwa wachezaji wa Bayern wamechoka kutokana na msongamano wa mechi. Dortmund walikuwa wamefungwa 2-0 baada ya Corentin Tolisso na Thomas Müller kuwaweka mabingwa hao wa Ulaya uongozini.

Erling Haaland aliwapa BVB goli la kwanza kisha akaongeza la pili ilipotimu dakika ya 55. Ushindi huu wa Bayern umekuja baada ya kichapo cha magoli 4 walichopokea katika Bundesliga mwishoni mwa wiki iliyopita mikononi mwa Hoffenheim.

DFL-Supercup | Bayern Munich v Borussia Dortmund | Tor Dortmund (2:2) (Andreas Gebert/Reuters)

Erlind Haaland akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli la kwanza la Dortmund

Mechi hiyo ambapo mshambuliaji wa TSG Hoffenheim Andrej Kramaric alipchika wavuni magoli mawili imezua tetesi kwamba Bayern sasa wanamuwinda mshambuliaji huyo raia wa Croatia. Ripoti zinaarifu kwamba Bayern wanamtaka Kramaric awe msaidizi wa mshambuliaji wao Robert Lewandowski ambaye alighadhabishwa sana na kushindwa huko mnamo Jumapili.

Gazeti la kila siku la Ujerumani Bild limeripoti kuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Hassan Salihamidzic aliwasiliana na wakala wa Kramaric baada ya kipigo hicho cha Jumapili.

 

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *