BASATA Wazungumza Kuhusu Lady Jaydee

October 8, 2020

 

Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Nago amesema kupitia Mwanasheria wao wamemtumia barua ya kutaka kuonana msanii mkongwe wa BongoFleva Lady Jaydee kuhusu wimbo wake ambapo inasemekana unahamasisha matumizi ya uvutaji bangi.

Kupitia mahojiano aliyofanya na EATV & EA Radio Digital, Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano wa BASATA Godfrey Nago amefafanua zaidi kuhusiana na hilo ambapo amesema.

“Kuhusu taarifa hizo naweza kusema nusu zina ukweli na nusu hazina ukweli kwa sababu bado hatujaita mkutano au kuongea na mtu yeyote kwenye hadhara kuhusu suala hilo, kitu ambacho tumefanya ni kumuita yeye kwanza na tayari tumeshampelekea barua kupitia Mwanasheria wetu ambayo anatakiwa aripoti hapa, halafu kuanzia hapo ndiyo tutakuwa na cha kuzungumza naye, huwezi kutoa hukumu kabla hujamzikiliza mtu”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *