Barwany ahaidi kuanza kushughulika na sekta za uvuvi, nishati na utalii iwapo atachaguliwa kuwa mbunge, on September 14, 2020 at 6:00 am

September 14, 2020

Na Ahmad Mmow, Lindi.Mgombea wa ubunge wa jimbo la Lindi kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi-CUF, Salum Barwany amehaidi ataanza na sekta za uvuvi, nishati na utalii ili ziwe natija kwa wananchi wa Lindi iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.Barwany alitoa ahadi hiyo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya kituo cha mabasi, kata ya Makonde, halmashauri ya manispaa ya Lindi.Barwany ambaye amepata kuwa mbunge wa jimbo hilo ( 2010-2015) kupitia chama hicho alisema licha ya kuendeleza mazuri aliyofanya katika kipindi chake cha ubunge ataanza na sekta za nishati, utalii na uvuvi ili wananchi wa jimbo hilo waweze kunufaika na fursa zinazotokana na sekta hizo.Alisema wananchi wa Lindi hawastshili kuendelea kuwa maskini wakati kuna bahari yenye samaki wengi wa aina tofauti, gesi asilia iliyopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara na vivutio vya utalii vilivyopo katika jimbo hilo la Lindi.Alisema akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha gesi asilia inawanufaisha wananchi wa jimbo hilo na mikoa ya Lindi na Mtwara. Kwani kama serikali ingekuwa na nia ya dhati ya kutaka wananchi wanufaike na gesi hiyo ingeweza. Hatahivyo haina dhamira hiyo japokuwa iliwapa matumaini makubwa Wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwamba ugunduzi wa nishati hiyo ungebadilisha maisha ya wananchi wa mikoa hiyo kiuchumi na miji ya Lindi na Mtwara ingekuwa kama Dubai.Alisema ahadi ya serikali kwa wananchi hao imesababisha baadhi yao kuingia kwenye madeni baada ya kukopa kwenye taasisi za fedha kwamatumaini kwamba wangeweza kulipa kupitia fursa ambazo zingetokanana nishati hiyo. Hata hivyo serikali imeachana na mradi huo. Badala yake imekuja na mradi wa umeme utakaotumia maji. Alisema mradi mpya wa bwawa la Julius Nyerere ni kielelezo cha serikali kuachana na mpango wa kuzalisha umeme wakutumia gesi asilia. Hivyo kuwaacha hewani wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara. Huku ikishindwa kurudi kwa wananchi kuwaeleza sababu za kuachana na mpango wa kuzalisha umeme kwakutumia gesi asilia.” Walichukuliwa mashehe, mapadre, wanasiasa na wananchi wakawaida kupelekwa Ulaya katika nchi ambazo zina gesi asilia wakajifunze na kuona faida ya gesi asilia. Lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea na haijarudi kuwaeleza wananchi kinaendelea nini. Mkinichagua nitakwenda kuhoji na kuhakikisha gesi asilia inawanufaisha wananchi wa Lindi na Mtwara,” Barwany akihaidi.Kuhusu sekta ya uvuvi alisema wananchi wa Lindi ambao wanatajwa kuwa ni wavivu wanategemea sekta ya uvuvi. Hata hivyo serikali imeshindwa kuwasaidia wavuvi. Kwani wavuvi wengi wanatumia zana duni za uvuvi. Kwani nkjambo lisilo la ajabu kuona wavuvi wengi wanatumia magogo ya miembe kusafiria baharini wakati wanavua. Huku alibainisha kwamba sekta ya uvuvi ingeweza kuwatoa kwenye lindi la umaskini linalosababisha waitwe wavivu iwapo serikali ingeamua kuwawezesha.Adha kuhusu sekta ya utalii alisema Lindi inavivutio vya utalii vya kipekee duniani ambavyo vinapatikana katika nchi chache. Alisema ni miji miwili pekee duniani ambayo bahari ipo juu na miji ipo chini. Akiitaja miji hiyo kuwa Athens uliopo Ugiriki na Lindi ulipo Tanzania. Hata hivyo maajabu hayo hayajawasaidia wananchi wa Lindi kupitia utalii. Kwani hakuna watalii wanaokwenda kuona maajabu hayo. Kwamadai kwamba serikali imeshindwa kutangaza kwakuwa yapo Lindi na mikoa ya kanda ya Kusini. Kwahiyo akiwa mbunge atahakikisha kivutio hicho cha utalii kinakuwa na tija kwa wananchi wa Lindi.Mgombea huyo alisema miradi mikubwa inayotekelezwa hivi sasa haina faida ya moja kwa moja kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ikilinganishwa na faida ambayo wangepata kutokanana gesi asilia, uvuvi na utalii.” Ndege, reli na bwawa la maji siyo mahitaji yetu. Kwasababu sisi hatuhitaji vitu vipya na hivyo hatunufaiki navyo. Uwanja wa ndege tulionao ulijengwa mwaka 1939 hadi 1945 lakini hizo ndege zilitua lini! reli tulikuwa nayo yakutoka Nachingwea kwenda Mtwara wakang’oa. Hilo bwawa la kufua umeme ni mbadala wa gesi asilia iliyopo huku. Sasa tushindwe kunufaika vikiwa huku tunufaike vikiwa huko?,” alihoji Barwany.Alisema mji wa Lindi ambao umechakaa ni ushahidi wa wazi kwamba hautakiwi kuwa na uzuri. Kwamadai kwamba mji huo ni miongoni mwa miji minne iliyopimwa miaka 1930. Akidai kwamba ulipimwa mwaka 1935. Kitendo kinacho onesha kwamba mji huo ulijengeka tangu miaka mingi. Lakini sasa wananchi wake wanaitwa wavivu na hawapendi maendeleo.Mwanasiasa huyo ambaye alianza rasmi kampeni zake hiyo jana alijinasibu kwamba miradi mingi ikiwamo barabara za lami katika mitaa ya Lindi, upanuzi wa bandari, taa za barabarani na kivuko imetokana juhudi zake akiwa mbunge. Hata hivyo baada ya yeye kuondoka hakuna miradi mipya. Kwani hata mradi wa ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango cha lami ambao unatekelezwa baada ya yeye kuondoka madarakani ni matunda ya jitihada zake.Barwani pia amehaidi akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha wananchi wa Ng’apa wanalipwa fidia kutokanana upanuzi wa barabara uliosababisha kukatwa minazi yao. Kitendo ambacho kimewasababishia umaskini.,

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Mgombea wa ubunge wa jimbo la Lindi kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi-CUF, Salum Barwany amehaidi ataanza na sekta za uvuvi, nishati na utalii ili ziwe natija kwa wananchi wa Lindi iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Barwany alitoa ahadi hiyo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya kituo cha mabasi, kata ya Makonde, halmashauri ya manispaa ya Lindi.

Barwany ambaye amepata kuwa mbunge wa jimbo hilo ( 2010-2015) kupitia chama hicho alisema licha ya kuendeleza mazuri aliyofanya katika kipindi chake cha ubunge ataanza na sekta za nishati, utalii na uvuvi ili wananchi wa jimbo hilo waweze kunufaika na fursa zinazotokana na sekta hizo.

Alisema wananchi wa Lindi hawastshili kuendelea kuwa maskini wakati kuna bahari yenye samaki wengi wa aina tofauti, gesi asilia iliyopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara na vivutio vya utalii vilivyopo katika jimbo hilo la Lindi.

Alisema akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha gesi asilia inawanufaisha wananchi wa jimbo hilo na mikoa ya Lindi na Mtwara. Kwani kama serikali ingekuwa na nia ya dhati ya kutaka wananchi wanufaike na gesi hiyo ingeweza. Hatahivyo haina dhamira hiyo japokuwa iliwapa matumaini makubwa Wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwamba ugunduzi wa nishati hiyo ungebadilisha maisha ya wananchi wa mikoa hiyo kiuchumi na miji ya Lindi na Mtwara ingekuwa kama Dubai.

Alisema ahadi ya serikali kwa wananchi hao imesababisha baadhi yao kuingia kwenye madeni baada ya kukopa kwenye taasisi za fedha kwamatumaini kwamba wangeweza kulipa kupitia fursa ambazo zingetokanana nishati hiyo. Hata hivyo serikali imeachana na mradi huo. Badala yake imekuja na mradi wa umeme utakaotumia maji. 

Alisema mradi mpya wa bwawa la Julius Nyerere ni kielelezo cha serikali kuachana na mpango wa kuzalisha umeme wakutumia gesi asilia. Hivyo kuwaacha hewani wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara. Huku ikishindwa kurudi kwa wananchi kuwaeleza sababu za kuachana na mpango wa kuzalisha umeme kwakutumia gesi asilia.

” Walichukuliwa mashehe, mapadre, wanasiasa na wananchi wakawaida kupelekwa Ulaya katika nchi ambazo zina gesi asilia wakajifunze na kuona faida ya gesi asilia. Lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea na haijarudi kuwaeleza wananchi kinaendelea nini. Mkinichagua nitakwenda kuhoji na kuhakikisha gesi asilia inawanufaisha wananchi wa Lindi na Mtwara,” Barwany akihaidi.

Kuhusu sekta ya uvuvi alisema wananchi wa Lindi ambao wanatajwa kuwa ni wavivu wanategemea sekta ya uvuvi. Hata hivyo serikali imeshindwa kuwasaidia wavuvi. Kwani wavuvi wengi wanatumia zana duni za uvuvi. Kwani nkjambo lisilo la ajabu kuona wavuvi wengi wanatumia magogo ya miembe kusafiria baharini wakati wanavua. Huku alibainisha kwamba sekta ya uvuvi ingeweza kuwatoa kwenye lindi la umaskini linalosababisha waitwe wavivu iwapo serikali ingeamua kuwawezesha.

Adha kuhusu sekta ya utalii alisema Lindi inavivutio vya utalii vya kipekee duniani ambavyo vinapatikana katika nchi chache. Alisema ni miji miwili pekee duniani ambayo bahari ipo juu na miji ipo chini. Akiitaja miji hiyo kuwa Athens uliopo Ugiriki na Lindi ulipo Tanzania. Hata hivyo maajabu hayo hayajawasaidia wananchi wa Lindi kupitia utalii. Kwani hakuna watalii wanaokwenda kuona maajabu hayo. Kwamadai kwamba serikali imeshindwa kutangaza kwakuwa yapo Lindi na mikoa ya kanda ya Kusini. Kwahiyo akiwa mbunge atahakikisha kivutio hicho cha utalii kinakuwa na tija kwa wananchi wa Lindi.

Mgombea huyo alisema miradi mikubwa inayotekelezwa hivi sasa haina faida ya moja kwa moja kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ikilinganishwa na faida ambayo wangepata kutokanana gesi asilia, uvuvi na utalii.

” Ndege, reli na bwawa la maji siyo mahitaji yetu. Kwasababu sisi hatuhitaji vitu vipya na hivyo hatunufaiki navyo. Uwanja wa ndege tulionao ulijengwa mwaka 1939 hadi 1945 lakini hizo ndege zilitua lini! reli tulikuwa nayo yakutoka Nachingwea kwenda Mtwara wakang’oa. Hilo bwawa la kufua umeme ni mbadala wa gesi asilia iliyopo huku. Sasa tushindwe kunufaika vikiwa huku tunufaike vikiwa huko?,” alihoji Barwany.

Alisema mji wa Lindi ambao umechakaa ni ushahidi wa wazi kwamba hautakiwi kuwa na uzuri. Kwamadai kwamba mji huo ni miongoni mwa miji minne iliyopimwa miaka 1930. Akidai kwamba ulipimwa mwaka 1935. Kitendo kinacho onesha kwamba mji huo ulijengeka tangu miaka mingi. Lakini sasa wananchi wake wanaitwa wavivu na hawapendi maendeleo.

Mwanasiasa huyo ambaye alianza rasmi kampeni zake hiyo jana alijinasibu kwamba miradi mingi ikiwamo barabara za lami katika mitaa ya Lindi, upanuzi wa bandari, taa za barabarani na kivuko imetokana juhudi zake akiwa mbunge. Hata hivyo baada ya yeye kuondoka hakuna miradi mipya. Kwani hata mradi wa ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango cha lami ambao unatekelezwa baada ya yeye kuondoka madarakani ni matunda ya jitihada zake.

Barwani pia amehaidi akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha wananchi wa Ng’apa wanalipwa fidia kutokanana upanuzi wa barabara uliosababisha kukatwa minazi yao. Kitendo ambacho kimewasababishia umaskini.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *