Barbara Gonzalez: Afisa mkuu mtenda wa Simba anavyobadili fikra za soka Tanzania.

September 17, 2020

  • Na Celestine Karoney
  • BBC Michezo Africa, Nairobi

Dakika 2 zilizopita

Barbara Gonzalez

Maelezo ya picha,

Barbara Gonzalez, Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Simba nchini Tanzania

Akikumbwa na shutuma kutokana na umri wake na jinsia, Barabara Gonzalez amezoea tangu alipoteuliwa mwanachama wa bodi ya klabu ya simba, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 alifanywa kuwa afisa mkuu mtendaji wa kwanza kuwahi kuteuliwa katika klabu yoyote nchini humo. Hatahivyo mashabiki wa klabu hiyo walio zaidi ya milioni 20 watasubiri kuona iwapo atafanikiwa ijapokuwa kwa muda mfupi ametakiwa kuthibitisha uwezo wake.

”Nimeenda katika mikutano miwili au mitatu ya ligi, ambapo wananitazama, wakifikiria, huyu mwanamke anajua nini, huyu kijana anajua nini”?, Gonzalez anaiambia BBC Michezo.

”Wananitazama na kudhania kwamba sio Mtanzania hivyobasi watanisengenya nami nawaangalia halafu ghafla nawapatia jibu kwa lugha yetu , wanarudi nyuma na inaishia hapo”. Majina ya babake na sura yake, huku babake akiwa ni raia wa Colombia – yaliwasumbua maafisa wengi wa soka ambao hawakujua kwamba Gonzalez amekulia mjini Dar es Salaam, mji mkuu wa kibiashara Tanzania.

Hatua Nzuri

Barbara Gonzalez

Maelezo ya picha,

Barbara Gonzalez anasema anahitaji kufanya kazi kwa bidii mara mbi zaidi ya wennzake wa kiume

”Nalazimika kufanya kazi mara mbili, sio kwasababu mimi ni mwanamke na kijana, lakini kwasababu sisi bado tuko Afrika ambapo heshima inawaendea wenye uzoefu na heshima nyengine inawaendea wanaume.

Baadhi ya mashabiki wa simba, akiwemo mbunge mmoja, wameuliza hadharani mbinu iliotumika kumteua Gonzalez – hususan ikilinganishwa na mtangulizi wake. ‘Katika kandanda kazi hizi bila kupendelea hupatiwa wanaume walio katika miaka ya 50 na 60 ambao wamekuwepo na hilo linaelezea jinsi Simba ilivyopiga hatua, ni kwa sababu hawataki kufanya kazi kama kawaida”, anasema Gonzalez. Senzo Mbatha kutoka Afrika ambaye aliondoka katika klabu ya Simba baada ya mwaka mmoja na kwenda kufanya kazi na wapinzani wao Yanga ana historia ya miongo miwili katika kandanda.

Uzoefu wake unaorodhesha kufanya kazi na klabu ya Afrika kusini ya Orlando Pirates miongoni mwa klabu kuu ambazo amefanya kazi nazo mbali na ligi ya Afrika kusini na kamati yake ya maandalizi ya kombe la dunia la 2010. Baada ya kuona uteuzi wa Mbatha, ushindani mkali unatarajiwa huku Simba ambayo mataji yake 21 ni sita chini ya Yanga, wanajaribu kuwafikia wapinzani wao wakuu – huku klabu ya Gonzalez ikifanikiwa kushinda mataji matatu yaliopita. Huku uzoefu wake wa kandanda ukiwa sio mkubwa sana kutokana na umri wake Gonzalez ana uzoevu mzuri.

Ana mengi kutoa

Barbara Gonzalez

Maelezo ya picha,

Barbara Gonzalez has an impressive CV having studied in the United States, England before returning to Tanzania

Baada ya kusomea uchumi nchini Marekani, na usimamizi wa kimaendeleo nchini Uingereza, kazi ya kwanza ya Gonzalez aliporudi nchini Tanzania 2014 alikuwa mshauri wa umma katika masuala ya kifedha.

Miaka miwili baadaye, alichukuliwa na bilionea wa Tanzania Mohamed Dewji, akifanya kazi kama mkuu wa wakfu wake na msimamizi wa wafanyakazi. Hatua hiyo ni pamoja na kufanya kazi na akaunti zilizoshirikisha mamilioni ya dola, ikiwemo moja iliokuwa na dola milioni 25, hivyobasi Dewji aliponunua asilimia 49 ya hisa za Simba 2017, alijua nani wa kumpatia kazi hiyo. Hatahivyo, alikataa wito wake wa kwanza, akiamini kwamba hayuko tayari wakati huo, lakini wiki iliopita alikuwa tayari.”Heshima huja unapotoa huduma nzuri na nilipojiunga na bodi, fikra zangu zilibadilika ndani ya miezi miwili ama mitatu kwasababu wanaona ninachoweza kufanya kila siku. Ongezeko la mapato – hiyo ndio sababu nimeletwa hapa”, anaelezea. ”Iwapo huwezi kuleta fedha na kuleta ubora katika kazi kama afisa mkuu mtendaji”, hufanyi kazi yako. ”Ya Pili ni kuimarisha nembo ya simba duniani – watu ni sharti waone kwamba klabu hii ni zaidi ya Tanzania. Tunajaribu kubadilisha sekta na kuona klabu kama chanzo cha kufanya biashara. Tuna mashabiki milioni 20 na jukumu letu ni kutafuta ushirikiano na biashara ili kuona jinsi tunavyoweza kuwabadilisha mashabiki hawa kuwa wateja kwa washirika wetu muhimu”.

Ni Mpenzi wa kandanda

Barbara Gonzalez

Maelezo ya picha,

Barabara Gonzalez anapenda sana mchezo wa kandanda na ni shabiki wa Arsenal

Baada ya kupenda soka kwa muda mrefu, hatua iliomfanya kucheza soka na kuipenda klabu ya Arsenal kutokana na babake, Gonzalez aliipuuza sekta hiyo kutokana na inavyochukuliwa barani Afrika. ”Jukumu langu ni kuifanya soka kuwa taaluma” , anasema. Kwa sasa inaonekana kama sekta isio na utaalam hilo linapaswa kubadilika”. Miongoni mwa vitu ambavyo analenga kufanya ni fursa ya kuimarisha talanta miongoni mwa vijana na ijapokuwa shirikisho la kandanda Tanzania linahitaji timu zote kuu kuwa na klabu za vijana ni timu mbili pekee zilizo na taasisi za kandanda za hakika. Simba tayari ina timu za wachezaji wasiozidi miaka 20 na wale wasiozidi miaka 17 lakini chuo cha mafunzo ya soka ndio mpango wa kwanza wa Gonzalez, anaelezea. ”Haingii akilini kwamba klabu kubwa kama Simba inanunua wachezaji mara kwa mara kutoka klabu zingine na ligi zingine”, anasema. Tunahitaji kutengeneza mpangilio ambao tutakuwa tunawakuza wachezaji kujiunga na timu kuu kila mwaka , lakini hilo litafanyika tu iwapo umewekeza pakubwa katika taaisi za mafunzo ya soka miongoni mwa vijana.

Pia unaweza kutazama

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Mtendaji mkuu wa Simba Barbara Gonzalez azungumzia uteuzi wake

Huku ushindani mkali na Yanga ukitarajiwa kutawala fikra za mashabiki wengi , Gonzalez anataka kuimarisha rekodi mbaya ya simba katika mashindano ya Afrika ambapo klabu hiyo imeshindwa kujimudu , mara ya mwisho ikifika nusu fainali ya kile kilichojulikana kama ligi ya mabingwa 1974. ”Lengo letu kuu kwa miaka michache ijayo ni kuwa mabingwa wa Afrika. Tunajua kwamba hilo haliwezi kufanyika kwa haraka” , anaelezea. ”Jukumu langu kutengeneza mazingira kwa benchi la kiufundi kuleta matokeo bora. Iwapo hilo litashirikisha kuwekeza katika wachezaji – tutawekeza vyema. Iwapo hiyo itashirikisha kuwekeza katika vifaa basi tutawekeza vyema. Iwapo tutalazimika kuwekeza katika lishe bora na vifaa vya matibabu ili kuleta matokeo bora – tutawekeza vizuri”. Gonzalez anataka kuwa mfano kwa wanawake wa Afrika ambao wanataka kuwa viongozi katika michezo.

”Nadhani hilo litawashinikiza wanawake wengine kusema: Wajua tuna barbra wetu huko , inawezekana kama anaweza kufanyakazi katika mazingira magumu kama vile Tanzania , nina hakika inawezekana katika maeneo mengine ya bara hili”, alimaliza.

Source link

,Na Celestine Karoney BBC Michezo Africa, Nairobi Dakika 2 zilizopita Chanzo cha picha, Barbara Gonzalez Maelezo ya picha, Barbara Gonzalez,…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *