Barbados kumuondoa Malkia Elizabath kama mkuu wa nchi, on September 17, 2020 at 8:00 am

September 17, 2020

Visiwa wa Barbados vimetangaza nia yake ya kumuondoa Malkia Elizabeth kama kiongozi wa nchi hiyo na kuwa Jamuhuri.”Muda umewadia wa kuachana na historia yetu ya kikoloni,” Serikali ya taifa hilo la kisiwa hicho cha Caribbean imesema.Ina lengo la kumaliza mchakato huo wakati wa kumbukumbu ya miaka 55 ya uhuru wake kutoka Uingereza, itakayofanyika mwezi Novemba mwaka 2021.Hotuba iliyoandikwa na Waziri Mkuu Mia Mottley imesema raia wa visiwa hivyo wanamtaka kiongozi mzawa.Kasri la Buckingham lilisema kuwa ni suala la serikali na watu wa visiwa vya Barbados.Chanzo cha habari katika kasri la Buckingham kimesema kuwa wazo hilo ”halikuja tu ghafla” na ” limekuwa likizungumzwa hadharani mara nyingi”, Mwanahabari wa BBC Jonny Dymond alisema.Waziri Mkuu wake ni Mia Mottley, alichaguliwa mwaka 2018 na mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.Kauli hiyo ilikuwa sehemu ya taarifa ya serikali ya kifalme, ambayo imetanabaisha sera za serikali na programu katika kuelekea vikao vipya vya bunge.Wakati ikisomwa na gavana mkuu, ina maana kuwa imeandikwa na Waziri Mkuu wa nchi.Hotuba hiyo pia ilinukuu onyo kutoka kwa Errol Barrow, Waziri Mkuu wa kwanza wa Barbados baada ya kupata uhuru, ambaye alisema kwamba nchi hiyo haipaswi “kurandaranda kwenye maeneo ya majengo ya wakoloni”.,

Visiwa wa Barbados vimetangaza nia yake ya kumuondoa Malkia Elizabeth kama kiongozi wa nchi hiyo na kuwa Jamuhuri.

”Muda umewadia wa kuachana na historia yetu ya kikoloni,” Serikali ya taifa hilo la kisiwa hicho cha Caribbean imesema.

Ina lengo la kumaliza mchakato huo wakati wa kumbukumbu ya miaka 55 ya uhuru wake kutoka Uingereza, itakayofanyika mwezi Novemba mwaka 2021.

Hotuba iliyoandikwa na Waziri Mkuu Mia Mottley imesema raia wa visiwa hivyo wanamtaka kiongozi mzawa.

Kasri la Buckingham lilisema kuwa ni suala la serikali na watu wa visiwa vya Barbados.

Chanzo cha habari katika kasri la Buckingham kimesema kuwa wazo hilo ”halikuja tu ghafla” na ” limekuwa likizungumzwa hadharani mara nyingi”, Mwanahabari wa BBC Jonny Dymond alisema.

Waziri Mkuu wake ni Mia Mottley, alichaguliwa mwaka 2018 na mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

Kauli hiyo ilikuwa sehemu ya taarifa ya serikali ya kifalme, ambayo imetanabaisha sera za serikali na programu katika kuelekea vikao vipya vya bunge.

Wakati ikisomwa na gavana mkuu, ina maana kuwa imeandikwa na Waziri Mkuu wa nchi.

Hotuba hiyo pia ilinukuu onyo kutoka kwa Errol Barrow, Waziri Mkuu wa kwanza wa Barbados baada ya kupata uhuru, ambaye alisema kwamba nchi hiyo haipaswi “kurandaranda kwenye maeneo ya majengo ya wakoloni”.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *