Barakoa yasababisha safari ya ndege kufutwa, on September 10, 2020 at 8:00 am

September 10, 2020

Safari ya ndege ya kampuni ya Canada WestJet ilifutwa na polisi kuitwa kwasababu mtoto alikuwa hajavaa barakoa.Safwan Choudhry anasema WestJet ilitaka mtoto wake mwenye umri wa miezi 19-avae barakoa, lakini mtoto huyo msichana aliendelea kulia.Ndege hiyo inasema suala hilo si la mtoto, ambaye ana umri wa chini wa mtu anayetakiwa kuvaa barakoa, bali linamuhusu mtoto wa miaka mitatu Bwana Choudhry.Jumanne asubuhi ndege chapa 652 iliyokuwa inatoka Calgary kuelekea Toronto ilisimamishwa na wasafiri wote wakaamrishwa kushuka.”Ni kitu ambacho sijawahi kukishuhudia,” Bwana Choudhry aliiambia BBC.Bwana Choudhry aliiambia BBC kuwa binti yake mkubwa, ambaye ana umri wa miaka mitatu, alikua anakula kitafunio kabla ya ndege kuondoka ndipo muhudumu wa ndege alipowakaribia akiwataka watoto wao wote wavae barakoa. Anasema yeye na mke wake walikuwa wamevaa barakoa.Alisema aliomba kama mtoto wake anaweza kumalizia kitafunio, lakini wakasema walikuwa na “sera ambayo haiwezi kuvumilia hilo” na hawatafunga milango ya ndege bila yeye kuvaa barakoa. Bwana anasema alikubali kuvaa mara moja.”Watoto wengi unahitaji kuwatuliza kwa namna fulani ambayo ndio njia ya kunyakua iPad kutoka kwao,”aliiambia BBC.Alisema kuwa binti yake wa miaka mitatu alivaa barakoa, baada ya kumlazimisha kwa nguvu.”Lakini binti yangu mdogo alikuwa na wakati mgumu, kimsingi alikuwa mgomvi.”Bwana Choudhry anasema alikasirika sana hadi akatapika.Anasema WestJet walikuwa wakali, na wakawaambia kwamba kwasababu binti yao mdogo hakuvaa barakoa, na amekasirishwa na kuvalishwa barakoa, familia yote itatakiwa kuondoka kwenye ndege.Anasema, waliwaambia kwamba kama hawataondoka, wanaweza kukamatwa, kushitakiwa na kuadhibiwa kifungo cha gerezani.Bwana Choudhry anasema yeye na mke wake walikuwa wenye heshima. Waliamua kukubali kuondoka kwenye ndege.Baadaye aligundua kuwa kwa mujibu wa sera ya usafiri ya Canada, ni watoto wenye umri wa zaidi ya miaka miwili wanaotakiwa kuvaa barakoa, kwa hiyo binti yake mwenye miezi 19 hakupaswa kuvaa barakoa.,

Safari ya ndege ya kampuni ya Canada WestJet ilifutwa na polisi kuitwa kwasababu mtoto alikuwa hajavaa barakoa.

Safwan Choudhry anasema WestJet ilitaka mtoto wake mwenye umri wa miezi 19-avae barakoa, lakini mtoto huyo msichana aliendelea kulia.

Ndege hiyo inasema suala hilo si la mtoto, ambaye ana umri wa chini wa mtu anayetakiwa kuvaa barakoa, bali linamuhusu mtoto wa miaka mitatu Bwana Choudhry.

Jumanne asubuhi ndege chapa 652 iliyokuwa inatoka Calgary kuelekea Toronto ilisimamishwa na wasafiri wote wakaamrishwa kushuka.

“Ni kitu ambacho sijawahi kukishuhudia,” Bwana Choudhry aliiambia BBC.

Bwana Choudhry aliiambia BBC kuwa binti yake mkubwa, ambaye ana umri wa miaka mitatu, alikua anakula kitafunio kabla ya ndege kuondoka ndipo muhudumu wa ndege alipowakaribia akiwataka watoto wao wote wavae barakoa. Anasema yeye na mke wake walikuwa wamevaa barakoa.

Alisema aliomba kama mtoto wake anaweza kumalizia kitafunio, lakini wakasema walikuwa na “sera ambayo haiwezi kuvumilia hilo” na hawatafunga milango ya ndege bila yeye kuvaa barakoa. Bwana anasema alikubali kuvaa mara moja.

“Watoto wengi unahitaji kuwatuliza kwa namna fulani ambayo ndio njia ya kunyakua iPad kutoka kwao,”aliiambia BBC.

Alisema kuwa binti yake wa miaka mitatu alivaa barakoa, baada ya kumlazimisha kwa nguvu.

“Lakini binti yangu mdogo alikuwa na wakati mgumu, kimsingi alikuwa mgomvi.”

Bwana Choudhry anasema alikasirika sana hadi akatapika.

Anasema WestJet walikuwa wakali, na wakawaambia kwamba kwasababu binti yao mdogo hakuvaa barakoa, na amekasirishwa na kuvalishwa barakoa, familia yote itatakiwa kuondoka kwenye ndege.

Anasema, waliwaambia kwamba kama hawataondoka, wanaweza kukamatwa, kushitakiwa na kuadhibiwa kifungo cha gerezani.

Bwana Choudhry anasema yeye na mke wake walikuwa wenye heshima. Waliamua kukubali kuondoka kwenye ndege.

Baadaye aligundua kuwa kwa mujibu wa sera ya usafiri ya Canada, ni watoto wenye umri wa zaidi ya miaka miwili wanaotakiwa kuvaa barakoa, kwa hiyo binti yake mwenye miezi 19 hakupaswa kuvaa barakoa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *