Balozi Wa Tanzania Awasilisha Hati Za Utambulisho Kwa Mfalme Wa Luxembourg

October 8, 2020

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji ambaye anawakilisha pia nchini Luxembourg, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme wa Luxembourg, Grand Duke Henri tarehe 2 Oktoba 2020.

Wakati wa hafla hiyo, Balozi Nyamanga na Mfalme Henri walifanya mazungumzo kuhusu umuhimu wa kuongeza wigo wa ushirikiano baina ya nchi mbili hizi na kutumia ipasavyo fursa mbalimbali zilizopo kwa ajili ya manufaa ya pande mbili. 

Miongoni mwa maeneo ya ushirikano yaliyojadiliwa ni pamoja na ushirikiano wa anga hususan ndege za mizigo, ushirikiano katika sekta za kifedha na kibenki na sekta ya madini hususan madini ya chuma kama yale ya Mchuchuma na Liganga, eneo ambalo Luxembourg ina uzoefu mkubwa.


 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *