Bahrain yaungana na UAE kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israel, on September 12, 2020 at 7:00 am

September 12, 2020

 Bahrain siku ya Ijumaa 11.09.2020 ilijiunga na Muungano wa falme za kiarabu katika kukubali kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israeli hatua iliyochochewa kiasi na hofu ya pamoja kuhusu Iran .Ikulu ya White House nchini Marekani imesema rais Donald Trump alitoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuzungumza kwa njia ya simu na mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.Akiwahutubia wanahabari katika ofisi yake, Trump aliitaja siku hiyo kuwa ya kihistoria na kwamba anaamini mataifa mengine yatafuata mkondo huo.Katika taarifa ya pamoja, Marekani, Bahrain na Israeli zimesema kuwa kufungua mawasiliano ya moja kwa moja na ushirikiano kati ya pande hizo mbili na chumi zilizoimarika kutaendelea kuleta mabadiliko ya manufaa katika eneo la Mashariki ya Kati na kuongeza uthabiti, usalama na ufanisi katika eneo hilo,

 

Bahrain siku ya Ijumaa 11.09.2020 ilijiunga na Muungano wa falme za kiarabu katika kukubali kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israeli hatua iliyochochewa kiasi na hofu ya pamoja kuhusu Iran .

Ikulu ya White House nchini Marekani imesema rais Donald Trump alitoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuzungumza kwa njia ya simu na mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.Akiwahutubia wanahabari katika ofisi yake, Trump aliitaja siku hiyo kuwa ya kihistoria na kwamba anaamini mataifa mengine yatafuata mkondo huo.

Katika taarifa ya pamoja, Marekani, Bahrain na Israeli zimesema kuwa kufungua mawasiliano ya moja kwa moja na ushirikiano kati ya pande hizo mbili na chumi zilizoimarika kutaendelea kuleta mabadiliko ya manufaa katika eneo la Mashariki ya Kati na kuongeza uthabiti, usalama na ufanisi katika eneo hilo

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *