Bahrain, UAE zasaini makubaliano ya kuwekeana ubalozi na Israel, on September 16, 2020 at 10:00 am

September 16, 2020

 Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu na Israel zimesaini makubaliano ya kihistoria ya kuwa na uhusiano wa kibalozi, katika sherehe iliyosimamiwa na rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House mjini Washington. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hatua hiyo inaweza kuwa mwanzo wa kumaliza kabisa uhasama kati ya nchi yake na mataifa ya kiarabu. Waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu Abdullah bin Zayed Al-Nahyan amemsifu Netanyahu, akisema amechagua amani kwa kusitisha unyakuaji wa ardhi za Wapalestina. Wapalestina wameyapinga makubaliano hayo, wakiyaita usaliti uliofanywa na mataifa ndugu ya kiarabu. Hata kabla ya kusainiwa, makubaliano hayo yalipingwa pia na Iran pamoja na Uturuki. Hadi sasa, Misri na Jordan yalikuwa mataifa pekee ya kiarabu yenye uhusiano wa kibalozi na Israel.,

 

Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu na Israel zimesaini makubaliano ya kihistoria ya kuwa na uhusiano wa kibalozi, katika sherehe iliyosimamiwa na rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House mjini Washington. 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hatua hiyo inaweza kuwa mwanzo wa kumaliza kabisa uhasama kati ya nchi yake na mataifa ya kiarabu. 

Waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu Abdullah bin Zayed Al-Nahyan amemsifu Netanyahu, akisema amechagua amani kwa kusitisha unyakuaji wa ardhi za Wapalestina. 

Wapalestina wameyapinga makubaliano hayo, wakiyaita usaliti uliofanywa na mataifa ndugu ya kiarabu. Hata kabla ya kusainiwa, makubaliano hayo yalipingwa pia na Iran pamoja na Uturuki. 

Hadi sasa, Misri na Jordan yalikuwa mataifa pekee ya kiarabu yenye uhusiano wa kibalozi na Israel.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *