Baada ya kumuonjesha Otile Brown Asali Vera Sidika ampa Buyu zima msanii Brown Mauzo

October 3, 2020

Mrembo Vera Sidika hayupo tena “Single”, imebainika sasa kuwa ni wazi yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi mbashara na msanii Brown Mauzo. Vera ambae amekua akigonga vichwa vya habari kwa maisha yake ya ustaarabu na hali ya juu, waingireza wangekunong’onezea kuwa ” She is living life on the first lane”.

Baada ya kuachana na msanii Otile Brown, Vera Sidika alipotea kwa mda kwenye upeo wa vichwa vya habari huku wote wapenzi hawa wawili wakiwa wanahaha kushindana kupata wendani wengine kimapenzi, lakini kwa bahati mbaya Otile Brown mahusiano yake ya pili na mchumba wake baada Vera Sidika mwenye asili ya Kiethiopia yalitumbukia nyongo huku pia Vera Sidika pia alikisiwa kumpata mchumba kutoka Nigeria lakini pia mahusiano yao hayakufikia malengo.

Picha ikionyesha Msanii Akothee  na Brown Mauzo wakiladenda hadharani kabla ya kutengana

Otile Brown akaugeukia muziki kama kipapasa mtima wake nakujituliza kwa kudondosha muziki na video kali zenye hadhi ya kimataifa. Kufikia hatua ya juzi kajipiga kifua kwa kutangazia umma kwa “Dusuma” ambayo ni video ya muziki ambayo alimshirikisha staa wa muziki anayeishi Marekani ila muzawa wa nchini Rwanda maarufu kama Meddy imefikia hatua ya kutazamwa mara milioni 10 ndani ya siku 90.

Lakini Vera Sidika ambae kwa upande mwingine amekua yupo mbioni kuonesha mashabiki mijengo yakifahari anayomiliki mjini Mombasa na baada ya mda kwenye ukimya na kuchoshwa na upweke, Vera Sidika ameamua kuliamsha popo kwa kumutangaza rasmi Brown Mauzo ambae ni msanii tajika nchini Kenya na ambae awali alishawahi fanya kazi na Alikiba kwenye kibao kinachofahamika kama “Nitulize” mwaka wa 2016. Ambapo ngoma hiyo aliitoa Brown Mauzo akiwa bado yupo kwenye mahusiano yakimapenzi na Madam Boss “Akothee” lakini haikuchukua mda baada ya kutoka kwa ngoma hii, mapenzi yao yakatumbukia nyongo na ikawa shida na balaa kwa Brown Mauzo ambapo ilionekana kuvunjika kwa uhusiano wao wa mapenzi na Akothee yalimurudisha nyuma sana Brown Mauzo kimuziki na kumupandisha juu Akothee. Japo Mauzo alitoa vibao vingine, lakini ilimchukua mda kurudi kwenye game kama ilivyokua awali hadi kufikia juzi alipotoa ngoma na rapper Timmy Tdat wa nchini Kenya kwa jina “Wote Wazuri” ambayo imekuja na baraka za kumuvisha pete ya uchumba mrembo Vera Sidika. Wakenya wamezidi kutoa hisia mseto kila kona kuhusu uhusiano huu wamapenzi baina ya Brown Mauzo na VeraSidika, lakini kunao watu wanaopinga mahusiano, watumiao msemo “Wataachana tu” na kunao wanao tumia msemo huu mpya mtaani unaosema “Mali safi acha iende cheni” kumtia moyo msanii Brown Mauzo ale asali bila uoga.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *