Ayoub: CCM imejitahidi kutekeleza Ilani yake kwa asilimia 100,

October 1, 2020

 

Na Thabit  Madai,Zanzibar.

MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kusini Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Ayoub Mohamed Mahmoud amesema kwamba Chama Cha Mapinduzi CCM kimejitahidi kutekeleza Ilani yake kwa asilimia 100 katika kuleta maendeleo ndani ya Mkoa huo.

Ayoub amesema sekta mbalimbali mkoani humo zimetatuliwa changamoto zao na wananchi wamenufaika kwa kuduma zilizobora Bora.

Kauli hiyo ameitoa leo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, Mkutano huo no muendelezo wa kampeni za Chama hicho.

Mjumbe huyo alisema,i kuwa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, umejitahidi katika kutatua changamoto katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya ambayo kwa sasa ndani ya Mkoa Kuna hospital kwa kila wilaya.

“Mkoa wa wetu wa Kusini kwa sasa unahospital kwa kila wilaya hii inatokana na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo wananchi hawana shida katika upande wa afya” akisema Ayoub.

Pia alisema,i kwamba katika sekta ya elimu Chama Cha Mapinduzi CCM kimejenga shule za ghorofa kwa kila wilaya ndani ya Mkoa huo ambapo kwa sasa wanafunzi wa kidato Cha tano na sita watasoma ndani ya Mkoa huo bila ya kwenda mjini.

“Kwa sasa vijana wetu watasoma hapa ndani ya Mkoa wa Kusini bila ya kwenda mjini kutokana na kujengwa kwa shule za ghorofa kwa kila wilaya hii inatokana na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM,” alisema Ayoub.

Alisema, ikwa upande wa huduma za jamii Chama Cha Mapinduzi CCM kimepeleka huduma ya maji Safi na Salam kwa kila shehia ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja.

Hata hivyo alisema kupitia Ilani ya Chama hicho kimejenga chuo Cha Amali ambapo vijana ndani ya Mkoa huo watapata fursa ya kujifujza ujuzi mbalimbali ambao utawasaidia katika kukuza kipato Chao Cha maisha.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *