Athari za kulala sana kwa mwanadamu, on September 19, 2020 at 7:40 pm

September 19, 2020

 Imebainika kuwa kulala zaidi ya masaa 9 usiku na zaidi ya dakika 90 wakati wa mchana kunaweza kuongeza hatari ya kupigwa na kiharusi.Matokeo haya yameonyeshwa kwenye jarida la “Neurology” lililochapishwa nchini China baada ya kuwafanyia utafiti watu 31,750 wenye umri wa takriban miaka 62.Mwanzoni mwa utafiti, iligundulika kuwa wale ambao hawakuwa na tatizo kupooza au shida zingine kubwa za kiafya ni wale wanaolala chini ya masaa nane ukilinganisha na wale ambao hulala masaa tisa.Hatari ya kupooza imeonekana kuongezeka  kwa asilimia 25 kwa watu ambao walipumzika kwa zaidi ya dakika 90 mchana mara kwa mara, ikilinganishwa na wale ambao walipumzika kwa saa isiyozidi moja au ambao hawakulala usiku.Utafiti pia umebaini kuwa wale ambao hulala kwa muda mrefu usiku na kulala muda mrefu wakati wa mchana wana uwezekano wa 85% ya kupooza.Wakati wa utafiti huo, watu walichunguzwa kwa muda wa miaka sita na 1557 kati yao walipooza kwenye harakati za kuchunguzwa.,

 

Imebainika kuwa kulala zaidi ya masaa 9 usiku na zaidi ya dakika 90 wakati wa mchana kunaweza kuongeza hatari ya kupigwa na kiharusi.

Matokeo haya yameonyeshwa kwenye jarida la “Neurology” lililochapishwa nchini China baada ya kuwafanyia utafiti watu 31,750 wenye umri wa takriban miaka 62.

Mwanzoni mwa utafiti, iligundulika kuwa wale ambao hawakuwa na tatizo kupooza au shida zingine kubwa za kiafya ni wale wanaolala chini ya masaa nane ukilinganisha na wale ambao hulala masaa tisa.

Hatari ya kupooza imeonekana kuongezeka  kwa asilimia 25 kwa watu ambao walipumzika kwa zaidi ya dakika 90 mchana mara kwa mara, ikilinganishwa na wale ambao walipumzika kwa saa isiyozidi moja au ambao hawakulala usiku.

Utafiti pia umebaini kuwa wale ambao hulala kwa muda mrefu usiku na kulala muda mrefu wakati wa mchana wana uwezekano wa 85% ya kupooza.

Wakati wa utafiti huo, watu walichunguzwa kwa muda wa miaka sita na 1557 kati yao walipooza kwenye harakati za kuchunguzwa.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *