Aston Villa yapata saini ya mlinda mlango aliyekuwa anakipiga Arsenal, on September 16, 2020 at 1:00 pm

September 16, 2020

 KLABU ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England imethibitisha kupata saini ya mlinda mlango aliyekuwa anakipiga Arsenal, Emiliano Martinez kwa mkataba wa miaka minne kwa dau la pauni milioni 16. Martinez, alisaini dili lake ndani ya Klabu ya Arsenal mara ya kwanza mwaka 2012 na amecheza kwa mkopo kwenye timu sita tofauti mpaka kufikia hatua ya kuuzwa jumla ndani ya Aston Villa kwa msimu wa 2020/21.Alikuwa anapewa nafasi ya kuwa kipa bora hapo baadaye ndani ya Arsenal kwa kuwa alianza kuaminika ndani ya kikosi hicho na alicheza kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA wakati Arsenal ikishinda mbele ya Chelsea msimu wa 2019/20.Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 28 amesema kuwa anafuraha kuwa ndani ya timu mpya na anaamini kwamba atafikia malengo ambayo amejiwekea yeye pamoja na timu.”Ninamshukuru Mungu kwa kuwa nimepata fursa wakati huu kwangu sio mbaya ikiwa ni muda mfupi wa kuwaonyesha mashabiki wa Arsenal kwamba nami nina kitu ninaweza kukifanya.”Ninawashukuru sana Arsenal kwa sapoti yenu ninarudia tena shukran kwa sapoti yenu kwa kuwa mmekuwa nami bega kwa bega mpaka hapa nilipofikia, wamenifanya sio nimekuwa kipa pekee hapana bali mchezaji mwenye furaha na furaha tena kubwa kwa ajili ya mashabiki na maisha yangu kiujumla,” amesema.Dean Smith, Meneja wa Aston Villa amesema kuwa wanatambua uwezo wake na wanaamini kwamba atakuwa katika wakati mzuri kwa kuwa alifanya hivyo hata alipokuwa ndani ya Arsenal. ,

 

KLABU ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England imethibitisha kupata saini ya mlinda mlango aliyekuwa anakipiga Arsenal, Emiliano Martinez kwa mkataba wa miaka minne kwa dau la pauni milioni 16. 

Martinez, alisaini dili lake ndani ya Klabu ya Arsenal mara ya kwanza mwaka 2012 na amecheza kwa mkopo kwenye timu sita tofauti mpaka kufikia hatua ya kuuzwa jumla ndani ya Aston Villa kwa msimu wa 2020/21.

Alikuwa anapewa nafasi ya kuwa kipa bora hapo baadaye ndani ya Arsenal kwa kuwa alianza kuaminika ndani ya kikosi hicho na alicheza kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA wakati Arsenal ikishinda mbele ya Chelsea msimu wa 2019/20.

Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 28 amesema kuwa anafuraha kuwa ndani ya timu mpya na anaamini kwamba atafikia malengo ambayo amejiwekea yeye pamoja na timu.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuwa nimepata fursa wakati huu kwangu sio mbaya ikiwa ni muda mfupi wa kuwaonyesha mashabiki wa Arsenal kwamba nami nina kitu ninaweza kukifanya.

“Ninawashukuru sana Arsenal kwa sapoti yenu ninarudia tena shukran kwa sapoti yenu kwa kuwa mmekuwa nami bega kwa bega mpaka hapa nilipofikia, wamenifanya sio nimekuwa kipa pekee hapana bali mchezaji mwenye furaha na furaha tena kubwa kwa ajili ya mashabiki na maisha yangu kiujumla,” amesema.

Dean Smith, Meneja wa Aston Villa amesema kuwa wanatambua uwezo wake na wanaamini kwamba atakuwa katika wakati mzuri kwa kuwa alifanya hivyo hata alipokuwa ndani ya Arsenal. 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *