ASEAN: China na Marekani zashutumiana kuchochea mizozo, on September 10, 2020 at 1:00 pm

September 10, 2020

China imeishutumu Marekani kuchochea mgogoro wa kijeshi katika ukanda wa bahari ya China Kusini, wakati mvutano baina ya nchi hizo mbili unaugubika mkutano wa kilele wa nchi Asia Pasifiki, ASEAN. Mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video unafanyika siku chache tu baada ya China kufyatua makombora katika eneo hilo la bahari linalozozaniwa, kama sehemu yake ya luteka za kijeshi kwenye eneo hilo, ambalo umiliki wake unadaiwa pia na Vietnam, Ufilipino, Malaysia, Brunei na Taiwan. Katika mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema malengo ya nchi yake katika Bahari ya China Kusini ni ya amani na utengamano, na kuongeza kuwa Marekani inanuia kuweka mivutano na kutafuta faida katika mizozo. Kwa upande mwingine, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema China inaendeleza tabia yake ya kuwatisha majirani katika eneo hilo muhimu la bahari.,

China imeishutumu Marekani kuchochea mgogoro wa kijeshi katika ukanda wa bahari ya China Kusini, wakati mvutano baina ya nchi hizo mbili unaugubika mkutano wa kilele wa nchi Asia Pasifiki, ASEAN.

 Mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video unafanyika siku chache tu baada ya China kufyatua makombora katika eneo hilo la bahari linalozozaniwa, kama sehemu yake ya luteka za kijeshi kwenye eneo hilo, ambalo umiliki wake unadaiwa pia na Vietnam, Ufilipino, Malaysia, Brunei na Taiwan. 

Katika mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema malengo ya nchi yake katika Bahari ya China Kusini ni ya amani na utengamano, na kuongeza kuwa Marekani inanuia kuweka mivutano na kutafuta faida katika mizozo. 

Kwa upande mwingine, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema China inaendeleza tabia yake ya kuwatisha majirani katika eneo hilo muhimu la bahari.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *