Amnesty International: Sheria zinatumika kukandamiza haki na uhuru Tanzania

October 13, 2020

Dakika 10 zilizopita

Amnesty

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limeikosoa serikali ya Tanzania kwa kutumia sheria kuminya uhuru na demokrasia.

Ripoti hiyo iliyopewa jina la ‘Ukandamizaji Kisheria kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania’ inadai kuwa, kutoka mwezi Januari mpaka Septemba 2020, kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukandamizaji vinavyoelekezwa kwa vyama vya kisiasa vya upinzani, vyombo vya habari vinavyokosoa, mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wanaharakati na watetezi wa haki za binaadamu.

“Ukandamizaji umekuwa na athari kubwa kwenye mijadala. Inaweza kuzuia ushiriki wa raia na kuzuia uchunguzi dhidi ya mamlaka katika rekodi za haki za binadamu, katika muktadha wa uchaguzi,” Inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Kuhusu madai ya ukandamizwaji wa vyama vya upinzani, ripoti hiyo inaeleza kuwa hata kabla ya kampeni, wanasiasa wa upinzani walikuwa katika wakati mgumu kwa kuzuiliwa kufanya mikutano ya hadhara na kukamatwa mara kwa mara na polisi.

“Wanasiasa wa upinzani wanaendelea kuripoti mashambulio dhidi yao, na hatua ya polisi kushindwa kuchunguza matukio hayo kwa haraka, undani na uwazi na kuchunguza, kunamaanisha kuwa uchaguzi wa Tanzania unafanyika wakati ambapo kuna ongezeko la uminywaji wa haki za wagombea na viongozi wa upinzani.”

Juhudi za kumpata Msemaji wa Serikali ya Tanzania Dkt Hassan Abbas kujibu tuhuma dhidi ya serikali hazikufanikiwa mpaka habari hii inachapishwa, na bado ingali anatafutwa.

Hata hivyo, hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi aliiambia BBC kuwa vyama vyote vya siasa nchini Tanzania vinavyoshiriki uchaguzi wa mwaka huu vipo huru na vinaendelea na kampeni.

“…hali ilivyo Tanzania ni tofauti na picha ambayo watu walioko nje ya Tanzania wanayo ama wanataka ionekane ilivyo.

Vyama vyote viko huru kufanya kampeni nchi nzima na hakuna ambaye amekamatwa kwa kufanya hivyo,” Waziri Kabudi aliiambia BBC Swahili mwezi Septemba alipokuwa akitoa ufafanuzi wa serikali juu ya taarifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ambaye katika taarifa yake alieleza kuwa kumekuwepo hali ya “kuongezeka kwa ukandamizaji wa kidemokrasia na haki za raia, nchini Tanzania.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya sauti,

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi aipinga vikali ripoti ya UN

“…hali ilivyo Tanzania ni tofauti na picha ambayo watu walioko nje ya Tanzania wanayo ama wanataka ionekane ilivyo.Vyama vyote viko huru kufanya kampeni nchi nzima na hakuna ambaye amekamatwa kwa kufanya hivyo,” Waziri Kabudi aliiambia BBC Swahili mwezi Septemba alipokuwa akitoa ufafanuzi wa serikali juu ya taarifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ambaye katika tarifa yake alieleza kuwa kumekuwepo hali ya “kuongezeka kwa ukandamizaji wa kidemokrasia na haki za raia, nchini Tanzania.

Ripoti ya Amnesty pia inaeleza kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na watetezi wa haki za binaadamu nchini Tanzania pia wanapitia katika wakati mgumu wa ukandamizwaji wa uhuru wa kufanya shughuli zao.

“Kuelekea uchaguzi, asasi zisizo za kiserikali ambazo zinaonekana kuwa zinaikosoa serikali zimekuwa zikitishiwa kufungiwa, ama zimefungiwa au kuzuiliwa kufanya shughuli zozote zinazohusiana na uchaguzi,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo”baadhi ya asasi zimepunguza ama kusimamisha kabisa kazi zake hali ambayo inaweza kutishia usimamizi wa haki za binaadamu katika uchaguzi.”

Ripoti hiyo imepigia mfano kuhusu Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC kusitisha shughuli zake kuwa kama sehemu ya ukandamizwaji unaofanywa na serikali kwa mashirika ya kiraia. THRDC ililazimika kufunga ofisi zake kwa muda kupisha uchunguzi wa polisi juu ya rekodi zao za kifedha.

Kuhusu suala la THRDC, hivi karibuni BBC ilifanya mahojiano na Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania Kamanda Simon Sirro ambaye alisema wanachunguza bilioni 6 za Tanzania zilizoingia katika akaunti ya THRDC:

”Kitengo chetu kinachohusika na mambo ya fedha haramu baada ya ufuatiliaji tuligundua kuwa kweli kuna fedha zimeingia nyingi, ukianzia Januari 2019 mpaka sasa mwezi wa nane takriban bilioni sita zimeingia kwenye hiyo akaunti, ndio tukataka kujua kama fedha hizo ni haramu, kikubwa zaidi zisije zikawa zimekuja kwa nia ovu.”

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya sauti,

Simon Sirro: Tunachunguza bilioni 6 za Tanzania zilizoingia katika akaunti hiyo

Amnesty International pia inaituhumu serikali ya Tanzania kwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari na matokeo yake ni kujengengeka “kwa hali ya hofu kwa wanahabari.

habari

” Uhuru wa vyombo vya habari pia ni eneo ambalo Kabudi alilizungumzia katika mahojiano yake na BBC akisema “Tanzania kuna uhuru wa habari …Sisi sio malaika, lakini tumefanya mengi katika sekta ya Habari mpaka kutunga sheria hizo ili kulinda maslahi ya mwandishi wa habari wa Tanzania.”

Katika ripoti hiyo, Amnesty imetoa rai kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa haki za binaadamu zinaheshimiwa kuelekea uchaguzi:

“Mamlaka isitishe kukamatwa kwa wanasiasa wa upinzani, kuwaruhusu kutumia vyombo vya habari na asasi za kiraia kufanya kazi kwa uhuru na kutoa uhuru kwa waangalizi kufuatilia na kuongea kuhusu masuala ya haki za binadamu.”

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *