Aliyeua Mwalimu, Afariki

September 10, 2020

FRANK Galimoshi (30), mkazi wa kata ya Chala wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amefariki dunia usiku wa kuamkia Septemba 3 mwaka huu, baada ya jitihada za kujiua, alipobaini kuwa amemuua mpenzi wake Mwalimu Tabitha Mwanyanje (29) kwa wivu wa kimapenzi kushindikana. Galimoshi siku za hivi karibuni, alifanya unyama mkubwa wa kumuua mpenzi wake kwa kumkata koo na sehemu kadhaa za mwili wake, kwa madai ya wivu wa kimapenzi ambapo naye alijaribu kujiua, lakini wananchi walijitokeza na kumzuia. Ilielezwa kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni kwamba, wawili hao walikuwa hawaaminiani katika mapenzi yao, ambapo wiki iliyopita wakiwa pamoja, mwanamke huyo ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Chalantai, simu yake iliingia meseji ya muamala wa mshahara. Meseji hiyo ilimpa shaka Galimoshi kwa kuhisi ni ya hawara wake, ndipo ugomvi ulipoanza, uliosababisha kifo cha mwalimu huyo na yeye kujidhuru kabla ya wananchi kujitokeza na kumpeleka hospitalini akiwa chini ya ulinzi. Wawili hao walidaiwa kutoaminiana katika maisha yao ya ndoa, baada ya mume kumtuhumu mkewe kuwa anachepuka na wanaume wengine, hali iliyosababisha achukue uamuzi maalumu wa kumuua kwa kumchoma kisu. Akiwa katika hospitali hiyo, usiku wa kuamkia Septemba 3 mwaka huu, Galimoshi alifariki dunia na tayari mwili wake ulikabidhiwa kwa familia, kwa ajili ya maziko. Samwel Kisingo mkazi wa Chala, alisema mauaji aliyofanya kijana huyo ni ya kikatili, hasa ikizingatiwa kuwa mwalimu huyo hakuwa mke wake, japokuwa walikuwa na watoto. “Hivi hawa vijana wamemsahau Mungu? Hivi unaweza ukafanya mauaji kwa ajili ya kukuta meseji tu, tena bila kuisoma?” Alihoji Kisingo. Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, ACP Justin Masejo alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo; kimoja cha mwalimu kuuawa kwa sababu ya kuingia meseji kwenye simu yake, na Galimoshi kufariki dunia kutokana na kujijeruhi. Kamanda Masejo alidai kuwa, baada ya Galimoshi kubaini kuwa amemuua mwalimu, naye alianza kujijeruhi kwa lengo la kujiua, kitu ambacho hakufanikiwa na alikamatwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu, lakini Septemba 3 alifariki dunia. “Jeshi la polisi linalaani tukio hilo na nawaasa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi. Endapo kama kuna tatizo, ni bora ufuate sheria kuliko kufanya mauaji kama alivyofanya kijana,

FRANK Galimoshi (30), mkazi wa kata ya Chala wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amefariki dunia usiku wa kuamkia Septemba 3 mwaka huu, baada ya jitihada za kujiua, alipobaini kuwa amemuua mpenzi wake Mwalimu Tabitha Mwanyanje (29) kwa wivu wa kimapenzi kushindikana.

 

Galimoshi siku za hivi karibuni, alifanya unyama mkubwa wa kumuua mpenzi wake kwa kumkata koo na sehemu kadhaa za mwili wake, kwa madai ya wivu wa kimapenzi ambapo naye alijaribu kujiua, lakini wananchi walijitokeza na kumzuia.

 

Ilielezwa kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni kwamba, wawili hao walikuwa hawaaminiani katika mapenzi yao, ambapo wiki iliyopita wakiwa pamoja, mwanamke huyo ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Chalantai, simu yake iliingia meseji ya muamala wa mshahara.

 

Meseji hiyo ilimpa shaka Galimoshi kwa kuhisi ni ya hawara wake, ndipo ugomvi ulipoanza, uliosababisha kifo cha mwalimu huyo na yeye kujidhuru kabla ya wananchi kujitokeza na kumpeleka hospitalini akiwa chini ya ulinzi.

 

Wawili hao walidaiwa kutoaminiana katika maisha yao ya ndoa, baada ya mume kumtuhumu mkewe kuwa anachepuka na wanaume wengine, hali iliyosababisha achukue uamuzi maalumu wa kumuua kwa kumchoma kisu.

 

Akiwa katika hospitali hiyo, usiku wa kuamkia Septemba 3 mwaka huu, Galimoshi alifariki dunia na tayari mwili wake ulikabidhiwa kwa familia, kwa ajili ya maziko. Samwel Kisingo mkazi wa Chala, alisema mauaji aliyofanya kijana huyo ni ya kikatili, hasa ikizingatiwa kuwa mwalimu huyo hakuwa mke wake, japokuwa walikuwa na watoto.

 

“Hivi hawa vijana wamemsahau Mungu? Hivi unaweza ukafanya mauaji kwa ajili ya kukuta meseji tu, tena bila kuisoma?”

 

Alihoji Kisingo. Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, ACP Justin Masejo alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo; kimoja cha mwalimu kuuawa kwa sababu ya kuingia meseji kwenye simu yake, na Galimoshi kufariki dunia kutokana na kujijeruhi.

 

Kamanda Masejo alidai kuwa, baada ya Galimoshi kubaini kuwa amemuua mwalimu, naye alianza kujijeruhi kwa lengo la kujiua, kitu ambacho hakufanikiwa na alikamatwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu, lakini Septemba 3 alifariki dunia.

 

“Jeshi la polisi linalaani tukio hilo na nawaasa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi. Endapo kama kuna tatizo, ni bora ufuate sheria kuliko kufanya mauaji kama alivyofanya kijana

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *