Aliyekuwa waziri wa nishati nchini Chad ashtakiwa kwa ufisadi, on September 6, 2020 at 6:00 pm

September 6, 2020

Waziri wa sheria nchini Chad Djimet Arabi amesema kuwa aliyekuwa waziri wa nishati nchini humo Djerassem Le Bemadjiel ameshtakiwa kwa wizi wa pesa za umma na kuagizwa kuzuiliwa.Le Bemadjiel alikamatwa siku ya Jumamosi baada ya malalamiko kutoka kwa taasisi moja inayoripoti moja kwa moja kwa rais wa nchi hiyo Idriss Deby ambaye amekuwa mamlakani tangu 1990.Chad sio taifa linalozalisha mafuta kwa wingi barani Afrika lakini mapato yanayotokana na mafuta yanachangia asilimia 40 ya pato jumla la taifa na asilimia 60 ya mapato ya maeneo kame katika taifa hilo. Mmoja wa mawakili wake amethibitisha kuwa mteja wake anashikiliwa na wanaandaa utetezi.Shirika la habari la Ufaransa la AFP limeripoti kuwa Le Bemadjiel aliyekuwa waziri wa nishati kati ya mwaka 2013 na 2016, anatuhumiwa kwa ufujaji wa pesa za umma, matumizi mabaya ya rasilimali za serikali na ufisadi.,

Waziri wa sheria nchini Chad Djimet Arabi amesema kuwa aliyekuwa waziri wa nishati nchini humo Djerassem Le Bemadjiel ameshtakiwa kwa wizi wa pesa za umma na kuagizwa kuzuiliwa.

Le Bemadjiel alikamatwa siku ya Jumamosi baada ya malalamiko kutoka kwa taasisi moja inayoripoti moja kwa moja kwa rais wa nchi hiyo Idriss Deby ambaye amekuwa mamlakani tangu 1990.

Chad sio taifa linalozalisha mafuta kwa wingi barani Afrika lakini mapato yanayotokana na mafuta yanachangia asilimia 40 ya pato jumla la taifa na asilimia 60 ya mapato ya maeneo kame katika taifa hilo. Mmoja wa mawakili wake amethibitisha kuwa mteja wake anashikiliwa na wanaandaa utetezi.

Shirika la habari la Ufaransa la AFP limeripoti kuwa Le Bemadjiel aliyekuwa waziri wa nishati kati ya mwaka 2013 na 2016, anatuhumiwa kwa ufujaji wa pesa za umma, matumizi mabaya ya rasilimali za serikali na ufisadi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *