Aliyekuwa mtangazaji maarufu wa televisheni Kenya azungumzia changamoto za kulemewa na maisha

October 2, 2020

Wiki iliyopita mitandao ya kijamii nchini Kenya ilitanda na taarifa kuhusu mmoja wa aliyekuwa mtangazaji maarufu wa televisheni kulemewa na maisha baada ya kustaafu. Lolani Kalu alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na weledi wake wa matumizi ya lugha ya Kiswahili, ufahamu wake wa tamaduni mbali mbali na kuwa na tajriba pana ya masuala ya sanaa kama ushairi, michezo ya kuigiza ya radio na televisheni.

Lakini kwa kipindi cha miaka kadhaa sasa, alipotea kutoka anga hizo za uandishi na usanii. Mtumizi mmoja wa mtandao wa TWITTER alimuulizia na hapo ndipo wengi wakatamani kujua yaliyomfika. Siku chache zilizopita, pekua pekua ya wadadisi wa mitandao ya kijamii aliibuka tena, japo kwa taarifa kuwa maisha kidogo yamemsibu.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *