Aliyekuwa Mfadhili wa Wasanii Ostadh Juma na Musoma afunguka kuhusu kufilisika

September 18, 2020

Meneja Ostadh Juma na Musoma amefunguka madai ya wasanii kumfilisi hadi kupelekea kuhama Jijini Dar Es Salaam na kuhamia Jijini Tanga, pia amesema asili ya watu wa Musoma wanafanya muziki kama starehe ila sio biashara.Akizungumza na eNewz ya East Africa Tv Meneja huyo ameeleza kuwa “Wasanii hawajawahi kunifilisi kwanza sanaa ya muziki nilikuwa nafanya kama starehe kwangu na ukiangalia asili ya watu wa Musoma wengi wao wanafanya muziki kwa starehe na sio biashara kwa sababu mimi hakuna pesa ya muziki ambayo nimewahi kula ila nimetumia pesa nyingi kusimamia muziki” Aidha Ostadh Juma na Musoma ameongeza kusema sio kwamba amefilisika ndiyo amehamia Tanga bali ameenda kwa ajili ya masomo, pia kabla ya kuja Dar Es Salaam alipitia mkoani humo na ndipo alipopewa jina la Ostadh.,

Meneja Ostadh Juma na Musoma amefunguka madai ya wasanii kumfilisi hadi kupelekea kuhama Jijini Dar Es Salaam na kuhamia Jijini Tanga, pia amesema asili ya watu wa Musoma wanafanya muziki kama starehe ila sio biashara.

Akizungumza na eNewz ya East Africa Tv Meneja huyo ameeleza kuwa “Wasanii hawajawahi kunifilisi kwanza sanaa ya muziki nilikuwa nafanya kama starehe kwangu na ukiangalia asili ya watu wa Musoma wengi wao wanafanya muziki kwa starehe na sio biashara kwa sababu mimi hakuna pesa ya muziki ambayo nimewahi kula ila nimetumia pesa nyingi kusimamia muziki” 

Aidha Ostadh Juma na Musoma ameongeza kusema sio kwamba amefilisika ndiyo amehamia Tanga bali ameenda kwa ajili ya masomo, pia kabla ya kuja Dar Es Salaam alipitia mkoani humo na ndipo alipopewa jina la Ostadh.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *